Carlos The Jackal
JF-Expert Member
- Feb 6, 2017
- 25,725
- 78,589
Haya mambo haya ndio yanafanya MTU akitwae Kiti hata kama ni Kwa Hila.
Kama Rais Samia ataishia 2030, Makamo wake atakubali habari zake za Siasa kuishia hapo, na kwa kua atakua keshajijenga, Mkutano Mkuu ukiamua kama ulivyoamua majuzi Mgombea kua Mmoja, itakuaje?
Kwa Kumtoa Mh Nchimbi kwenye Ukatibu Mkuu, wamemuondolea nguvu kwenye Chama, ni kweli.
Pia soma: Wajumbe Mkutano Mkuu CCM wapitisha Rais Samia, Dkt. Mwinyi kugombea Urais 2025
Kumuweka Mzee Wassira Makamo, na hatimaye Katibu Mkuu mpya ambaye naye atakua na Itikadi sawa na za Akina Wassira, nikama vile CCM inarudisha chama kwenye zile Itikadi za Mwalimu Nyerere. Je, ni Kwa ajili ya 2025 hii au au 2030?
Na kama ni Kwa ajili ya 2030, nani ajuaye yalotokea 3/2021 kua hayawez kujirudia na hatimaye Msiyependa kua Mwenyekiti ndio akawa na kuvuruga mipango yote?
Hapa ndipo Palipo na udhaifu wa Katiba ya CCM, kwamba Rais hapohapo ndio anakua Mwenyekiti wa CHAMA. Nadhani hii pia imefanya Chama kishindwe kuwawajibisha Viongozi wabadhirifu, wazembe, Mafisadi, Wenye Undugu) kwa sababu unakuta Wana Mahusiano na Rais ambaye pia ni Mwenyekiti.
Turudi kwenye Hoja ya msingi, Mh. Nchimbi atakubali na ataishia 2030? Uchaguzi wa 2030, Fomu zitakua Kwa anayetaka?
Ama kweli uchaguzi 2025 Kwa CCM hautabiriki, ni Ama Dola imeshindwa kusoma alama za nyakati ya kile kinachoendelea huku mtaani na kuisaidia CCM au Dola yenyewe imeichoka CCM na imeamua kwenda na Lissu.