Uchaguzi Mkuu wa 2025 unakaribia. Rais Samia Suluhu Hassan anaonekana kuwa na nafasi kubwa ya kushinda na moja ya silaha zake kuu ni aina ya wagombea ubunge waliopitishwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Wagombea Wenye Ushawishi
CCM imepitisha wagombea wanaopendwa na wananchi na wenye historia ya kujituma majimboni, wengine wamejijengea heshima kwa kusikiliza matatizo ya watu na kuyatafutia suluhu, hii inaleta mvuto kwa wapiga kura na kumsaidia Rais kupata kura nyingi.
Mchanganyiko wa Vijana na Wazee
Wagombea waliochaguliwa si wa kundi moja, kuna wanasiasa wenye uzoefu wa muda mrefu na pia vijana wapya wenye fikra za kisasa, hii inakipa chama sura ya upya huku kikibaki imara, Rais Samia anafaidika kwa kuwa na timu yenye nguvu tofauti.
Kuimarisha Ajenda ya Maendeleo
Wagombea wengi wanahusiana moja kwa moja na miradi ya maendeleo, wanaelewa vipaumbele vya serikali ya Samia, kama diplomasia ya uchumi, elimu, afya na miundombinu. Hii itarahisisha utekelezaji wa Ilani na kushawishi wapiga kura kuunga mkono CCM.
Taswira ya Mwanamke Kiongozi
Rais Samia pia ameweka msisitizo kwa wagombea wanawake, hatua hii inaonyesha dhamira yake ya kuleta usawa wa kijinsia. Inamjengea heshima zaidi na kuvutia wapiga kura, hasa vijana na wanawake.