Rais Samia atengua uteuzi wa Albert Chalamila RC Mwanza, Dkt. Batilda ateuliwa kuwa RC Tabora

Ukisikiliza hutuba yake nzima alimaanisha hayi mabango waende nayo ofisi kwake hata wakiandika matusi waende nayo kwake sio siku ya ziara ya Rais ..
Sasa sielewi kwanini watu wamekata kipande kidogo !!
Hata kama ni ofisini kwake. Je kama mabango mengine ya matusi yangemlenga Rais, waziri au kiongozi mwingine ingekuwaje? maana watu vichwa vimepata moto na ruhusa ndo keshatoa Chalamila.
 
Sasa Mama anatumbua kwa hasira. Hii so sawa. Alitakiwa aisikilize hotuba yake yote. Siku hizi editors wamejaa kila Kona.

Ingawa pengine inawezekana Kuna sababu ingine
Hujamwelewa mama naona.
Wakati wa kuwaapisha, alimuambia kijana kwamba ni mlipukaji (isomeke mropokaji) na akampa angalizo. Nadhani hii ya jana ni chagizo tu la kilichokuwa tayari kipo mezani. Kwa hio hajahukumiwa ka kosa la jana tu, ana mengine.
 
Ukisikiliza hutuba yake nzima alimaanisha hayi mabango waende nayo ofisi kwake hata wakiandika matusi waende nayo kwake sio siku ya ziara ya Rais ..
Sasa sielewi kwanini watu wamekata kipande kidogo !!
Weka hicho kipande chote.
 
Kuna clip inaonyesha akihimiza wananchi wakampokee Rais Samia Mwanza akawaambia ni ruhusa pia kubeba mabango hata kama yameandikwa matusi
Inshort jamaa,alikuwa anajua anytime ataliwa head,hata yeye hakuwa ok kuendelea kuwa konda wa Basi linalomilikiwa na tajiri ,ambae kimsingi Hana Imani nae!
 
Mama anajibainisha kama kiongozi asiyetaka mbwembwe! Wote wanaotaka mbwembwe wakaunde makundi ya sanaa za vichekesho kwani nayo ni shughuli halali na pia yenye kuelimisha jamii, lakini kutumia u-RC kufanya hivyo HAPANA.

By the way, Mama alimchelewesha sana huyu. Kati ya teuzi za Wakuu wa Mikoa zilizolalamikiwa ni pamoja na uteuzi wa Chalamila. Ni kati ya viongozi walioipa hekima "likizo isiyo na malipo". Kila kinachomjia kinywani hukitamka pasi na tafakari angalau ya kawaida.

ASANTE MAMA, UMEZIDI KUTUFURAHISHA. BADO ALLY HAPI.
 
uongozi ni dhamana.
uongozi ni sawa na koti la kuazima.
hakuna mwenye hati miliki.
jambo la msingi ni kwa viongozi wetu wasiwaonee walio chini yao, wawatendee haki.
tusipende kutoa kadi nyekundu kabla ya kutoa ya mjano.
lkn pia tusipende kusikiliza sana majungu na fitina, tutajikuta yunawaadhibu viongozi walio bora na kubaki na watendaji wanafaiki na wazandiki.
tuwe makini.
mfano; kuna wakati mmoja Rais mstaafu JK kwa kauli yake alisema; aliwahi kufukuza kazi kiongozi mmoja lkn badae alipo kuja kufanya uchunguzi alibaini kumbe yalikuwa majungu na fitina, alisikitika sana, maaana yake ni kwamba kila kiongozi ktk nafasi yake awe makini kabla ya kutoa hukumu.
naaamini hata Rais wetu Mama Samia mara zote hufanya "duediligence" kabla ya kufanya maamuzi.
kazi iendelee.....jambo la msingi wananchi wanataka maendeleo.
 
nimeipenda sana Style ya uongozi wa Amiri Jeshi Mkuu Mama Samia,
hakika ameonyesha kuwa cheo ni dhamana, leo unacho kesho huna, hivyo usitegemee kuzikwa na cheo.
kuna jambo la kujifunza kwa wateule wote, badilikeni msiishi kwa mazoea.
 
Hii ni Danganyika Mkuu
 
Ni mwehu tuu anaweza kusikiliza bunge la ccm.kungekua na nondo za kina lisu, msigwa,mdee etc etc tungesikiliza
Ni suala la maisha yako!

Kelele mnazopiga kwa chalamila mnezipiga pia kwa mambo ya hovyo yakiyopitishwa kwenye bajeti mngekuwa na akili!

Chalamila katoka na haina maana yeyote kwako ila bajeti ile ipo mpaka 2022. Ndio mtajua hamjui mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…