Rais Samia atengua uteuzi wa Albert Chalamila RC Mwanza, Dkt. Batilda ateuliwa kuwa RC Tabora

Bajeti kajadili na mkeo. Habari ya mjini ni kutenguliwa kwa Chalamila.
 
Bajeti kajadili na mkeo. Habari ya mjini ni kutenguliwa kwa Chalamila.
sina mkee dadekii, labda nije jadili na mkeo geto kwanguuu ila unajua ishu ya Chalamila bana ka kajitakia mwenyewee so tumwache na akili zake
 
Wewe mwenye akili mbona hatujawahi kuousikia umesimamisha bajeti kupitishwa baada ya wewe na mkeo kuijadili chumbani kwako? Acha kujitukuza wewe.
Usioneshe umbumbumbu wako mbele ya watu namna hii

Ni aibu hata kwa mimi mmeo
 
Your browser is not able to display this video.

Duuh Chala boy
 
Mama akomaa kutupa nje ya injini vipuri vibovu. "Magu legacy in the toilet".
 
Lkn huyu Jamaa mm naona alitaka mwenyewe kutumbuliwa mtu mwenye akili timamu unaweza sema maneno yale mbele ya wahandishi wa habari kweli?

Eti wananchi RUKHSA kubeba MABANGO na andikeni chochote HATA MKITAKA kuandika MATUSI hivi kweli RC hajui ya kwamba sio kila RAIA anaweza kumpenda RAIS, na anaweza kuchukuwa hiyo Advatage ya kupeleka ujumbe wenye matusi au maneno yasio kuwa na utu mbele ya RAIS.
 
Alikuwa ni Mhadhili Msaidizi kwenye moja ya chuo kikuu kimoja wapo Mkoani Iringa. Ni maarufu sana Iringa kwa uimbaji wake wa nyimbo za Kihehe. Na ni Mnyalukolo wa kutokea Wilayani Mufindi bila shaka.
Ongeza juhudi kujifunza kiswahili kizuri. ...."kwenye moja ya chuo kikuu kimoja wapo"...........
 
Kasema waende ofisini kwake na hayo mabango wakatoe kero zao sio waende na mabango kwa mama akija...
Sijui kwa nini kimekatwa kipande hicho tu
Wafitini ni wengi. Wenye haki uzongwazongwa na wasio haki.
 
Challamila mm binafsi nakutakia kila la kheri kule uendako pumuzika tuliza akili songa mbele.Kazi yeyote ya kuteuliwa ina matokeo hayo,wewe ni msomi mzuri hakuna Diploma au degree ya Ukuu wa Mkoa,miaka Tisa sio mingi wewe bado kijana,kaa na adui zako mbali usimsahau Mungu wako.
 
'Taarifa iliyotolewa usiku huu wa Juni 11, 2021 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jaffar Haniu imesema katika'
Juni 11 usiku mbona haujafika?
 
Duh Chalamila kaliwa kichwa, pombe itanywekwa kweli? Haha

chalamila hakuliwa kichwa ila yeye mwenyewe kafanya kusudi ili atolewe. chalamila ukimzingua anakuzingua mama alimzingua chalamila petrol na kiberiti chalamila akaona isiwe tabu si wewe hupendi mabango mimi nawaeleza wananchi waje na mabango tena hata ya kukutukana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…