Jasmoni Tegga
JF-Expert Member
- Oct 28, 2020
- 12,624
- 24,751
Ndiyo kusema ni eneo ambalo wazalendo wanaharibikia?ndugu yangu hata ukiweka wachungaji na maaskofu pesa itapigwa tu, TPA ndiyo jiko la nchi Mkuu msosi wote unapikwa hapo - yaani pesa inakutafuta wewe sasa ufanyaje.
Huko Msd unafikiri waliharibu kihivyo basi.Wajeda waliboronga msd..hapo ndio wataboronga zaidi.
Tuazime nchi za wenzetu managers wa bandari zinazofanya vzr duniani.
#MaendeleoHayanaChama
Itakusaidia nini wewe kama wewe?Hongera sana Plasduce Mbossa kwa uteuzi, tunaomba mwenye CV ya Mbossa please
Kwamba wenye mamlaka nao hawajui la kufanya? Nadhani ni wakati mwafaka sasa wananchi tufanye jambo letu! 🙂RAISI ANALALAMIKA
Matatizo hayako bandarini peke yake.Huyu bwana si alimteua yeye? masikini sijui kakosea nini? Itajulikana tu
Au vice versa. Kinachotakiwa kujulikana ni nani mshika-usukani?'Mama' hapindui kwa Mswahili.
Kinda interested to know ^those fools^but not those 'Fools' of yours
Rais Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Ndgu. Eric Hamisi. Nafasi yake inachukuliwa na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Ndgu. Plasduce Mkeli Mbossa.
Huo mfumo utobolewe mara moja.Muundo upo sawa; tatizo politics, kama si mtu wa mfumo huwezi kudumu kwenye nafasi yako
Ninasikitika kidogo kukubaliana na wewe kuhusu "Kubinafsisha", lakini sikubaliani nawe kama kubinafsisha huko kutaishia bandarini. Mimi ningependa hata sehemu anayoishikilia huyo anayeteua hawa wezi/wazembe, sehemu hiyo pia IBINAFSISHWE.Binafsisha hizi BANDARI, naona zinatupa shida kubwa kuziendesha au recruits freshers kutoka University, peleka wachache pale Durban, Capetown, Rotterdam, Botswana (dry port)wakajifunze kwa 24mth kuhusu uendeshaji wa hizi bandari, na ajira mpya zifanyike yaani we need to start upya
Kamkabidhi Kagame familia yako..sio Bandari ya nchi hii.Hii bandari wamkabidhi kagame.
Au wazungu wawe top managers.
#MaendeleoHayanaChama
Tufike mahali tuache maigizo haya tunayofanyiwa mara kwa mara na hawa watu wote, hao wanaotenguliwa na wanaowatengua.What do you expect? Apelekwe kisutu mahskamani haraka.
Bandari zote zenye ufanisi huko Duniani zimebinafsishwa,ujuaji na ushkaji mavi wa Kibongo ndio unaleta hasara tuu.Ikibinafsishwa ndio inakufa kabisa. Rejea kilichowahi kutokea kwenye Reli, Shirika la ndege na viwanda
Nani kasema Director ndio alifanya madudu pekee,yeye ndio alitakiwa kuifumua hiyo safu yake ya watumishi na hakufanya hivyo so anawajibishwa yeye.Sasa kumtumbua na kumuweka aliyekuwa kaimu wake ndio suluhisho la tatizo?
Bandari inatakiwa ifumuliwe kuanzia chini kabisa mpaka kileleni. Hii mambo ya kuondoa mtu mmoja mmoja huku kuacha mashina na mizizi ni ujinga tu.
Ni ngumu kuamini kama kuna madudu basi yalifanywa na Mkurugenzi peke yake. Kwa vyovyote ni kwa msaada mkubwa wa waliokuwa chini yake. Sasa leo hii ukisema unamuondosha mkurugenzi na kuacha walio chini yake ambao kiuhalisia ndio watekelezaji wakuu wa hayo madudu hapo unakuwa umefanya nini?
Hiki kinachofanyika ni sawa na kuzima moto kwa kutumia mabua, kwa juu unaona kama moto umezimika ila chini unafukuta vile vile.
Aisee DPP na wenzie hawana hurumaYuko huku!👇👇
Dar es Salaam. Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Madeni Kipande (66) amesomewa mashtaka ya kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh4.2 bilioni akiwa amelazwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI), Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Amesomewa mashtaka akiwa kitandani leo Jumatatu Julai 4, 2022 baada ya kufanyiwa upasuaji wa mgongo katika hospitali hiyo.
Hatuna proffessionalism.Bandari bado wahusika wanashindwa kuteua watu educated na experienced na mambo ya bandari. Wapo wasomi wazuri pale DMI wengine mpaka wamestaafu akina Mzee Mayagilo hawa wameanza kwenye Ubahari to Marine engineering to Management PHDs.
Serikali inahitaji kuwekeza kwenye Teknolojia ambayo italeta newly improved controls. Mfano Port of Durban .
Suala la Hamisi kwa uzoefu wangu na hisia ni kwamba alijitahidi kutenda na kujali wafanyakazi lakini pia alikula kwa kamba yake ila kilichomtoa pale ni kwamba kuna matajiri fulani ambao wanafanya shughuli zao za mizigo wameibuka awamu hii ya mama nadhani alishindwa kwenda nao sawa wakaamua wamwage ugali kwa bosi wake. Bandarini kuna matajiri hawa kama hawa wanaofadhili team ya wananchi wale kama hutoweza kwenda nao sawa wanauwezo wa kukujengea fitina ukatolewa wale huwa mazungumzo yao ni magogoni, kwa katibu au kwa mzee wa uongo wakisha kuchongea huko lazima utatolewa tuu.
Nadhani kazi hiyo ingetangazwa na watanzania wenye vigezo wakaiomba. Yupo kijana wa Liundi anapiga sana kazi pale TPA kama Business dev manager sijui au Port manager. Wapo wasomi wamepita DMI wamekaa scandinavia na wamecheza na bandari wanajua nini kifanyike tusione ubaya kuchukua diasporas.