Rais Samia atengua uteuzi wa Eric Hamissi, Mkurugenzi Mkuu wa Usimamizi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA)

Rais Samia atengua uteuzi wa Eric Hamissi, Mkurugenzi Mkuu wa Usimamizi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA)

ndugu yangu hata ukiweka wachungaji na maaskofu pesa itapigwa tu, TPA ndiyo jiko la nchi Mkuu msosi wote unapikwa hapo - yaani pesa inakutafuta wewe sasa ufanyaje.
Ndiyo kusema ni eneo ambalo wazalendo wanaharibikia?
 
Wajeda waliboronga msd..hapo ndio wataboronga zaidi.

Tuazime nchi za wenzetu managers wa bandari zinazofanya vzr duniani.

#MaendeleoHayanaChama
Huko Msd unafikiri waliharibu kihivyo basi.
Nchi hii watu wakiamua kukutengenezea zengwe HUCHOMOKI. Watu ni mafundi bwana, na wakiamua kuiaminisha Public ujue hakuna atakayeamini kuwa hujaharibu.

Ukitaka kujua ukweli wewe subiri uone kinachofuata baada ya kutenguliwa mtu kwa tuhuma nzito. Je inakwenda mahakamani au kimyaaaaa!
 
Huyu bwana si alimteua yeye? masikini sijui kakosea nini? Itajulikana tu
Matatizo hayako bandarini peke yake.

Matatizo yapo kila mahala, hata kwa wateuzi wenyewe.

Sasa jiulize, hapa katoa usuluhishi gani juu ya tatizo lililopo bandarini.

Huyu bwana mdogo aliyeteuliwa naye siku chache zijazo utasikia kishashindwa kazi.

Mbaya zaidi ni kutochukua muda kufahamu tatizo la sehemu hiyo hasa ni lipi, linalofanya pawe na 'turnover' kubwa kiasi hiki?
 
Rais Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Ndgu. Eric Hamisi. Nafasi yake inachukuliwa na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Ndgu. Plasduce Mkeli Mbossa.

Eric Hamissi,ndiye aliyeiuaTanzania Investment bank ( TIB) , mkaja kumpa Kuwa mkurugenzi Mkuu wa Usimamizi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) . What do you expect? Apelekwe kisutu mahskamani haraka.​

Binafsisha hizi BANDARI, naona zinatupa shida kubwa kuziendesha au recruits freshers kutoka University, peleka wachache pale Durban, Capetown, Rotterdam, Botswana (dry port)wakajifunze kwa 24mth kuhusu uendeshaji wa hizi bandari, na ajira mpya zifanyike yaani we need to start upya
Ninasikitika kidogo kukubaliana na wewe kuhusu "Kubinafsisha", lakini sikubaliani nawe kama kubinafsisha huko kutaishia bandarini. Mimi ningependa hata sehemu anayoishikilia huyo anayeteua hawa wezi/wazembe, sehemu hiyo pia IBINAFSISHWE.
Kwa maana halisi, nitakubaliana nawe moja kwa moja kama serikali yote itabinafsishwa, kwa maana ndiyo iliyoshindwa kila kazi, hata kazi ya kuhakikisha kwamba haya mashirika yake na watendaji wote wanafanya kazi kwa ufanisi.

I am deadly serious about this.
 
What do you expect? Apelekwe kisutu mahskamani haraka.
Tufike mahali tuache maigizo haya tunayofanyiwa mara kwa mara na hawa watu wote, hao wanaotenguliwa na wanaowatengua.
Hivi inakuwaje mara zote watu wanatenguliwa, na haielezwi sababu za kutenguliwa kwao?
Kama wametenguliwa kwa kufanya makosa yanayohusiana na uhujumu wa eneo lao la kazi, kwa nini iishie katika kutenguliwa peke yake bila ya kufikishwa mbele za sheria kujibu uhujumu waliofanya!
 
Bandari bado wahusika wanashindwa kuteua watu educated na experienced na mambo ya bandari. Wapo wasomi wazuri pale DMI wengine mpaka wamestaafu akina Mzee Mayagilo hawa wameanza kwenye Ubahari to Marine engineering to Management PHDs.

Serikali inahitaji kuwekeza kwenye Teknolojia ambayo italeta newly improved controls. Mfano Port of Durban .

Suala la Hamisi kwa uzoefu wangu na hisia ni kwamba alijitahidi kutenda na kujali wafanyakazi lakini pia alikula kwa kamba yake ila kilichomtoa pale ni kwamba kuna matajiri fulani ambao wanafanya shughuli zao za mizigo wameibuka awamu hii ya mama nadhani alishindwa kwenda nao sawa wakaamua wamwage ugali kwa bosi wake. Bandarini kuna matajiri hawa kama hawa wanaofadhili team ya wananchi wale kama hutoweza kwenda nao sawa wanauwezo wa kukujengea fitina ukatolewa wale huwa mazungumzo yao ni magogoni, kwa katibu au kwa mzee wa uongo wakisha kuchongea huko lazima utatolewa tuu.

Nadhani kazi hiyo ingetangazwa na watanzania wenye vigezo wakaiomba. Yupo kijana wa Liundi anapiga sana kazi pale TPA kama Business dev manager sijui au Port manager. Wapo wasomi wamepita DMI wamekaa scandinavia na wamecheza na bandari wanajua nini kifanyike tusione ubaya kuchukua diasporas.
 
Sasa kumtumbua na kumuweka aliyekuwa kaimu wake ndio suluhisho la tatizo?

Bandari inatakiwa ifumuliwe kuanzia chini kabisa mpaka kileleni. Hii mambo ya kuondoa mtu mmoja mmoja huku kuacha mashina na mizizi ni ujinga tu.

Ni ngumu kuamini kama kuna madudu basi yalifanywa na Mkurugenzi peke yake. Kwa vyovyote ni kwa msaada mkubwa wa waliokuwa chini yake. Sasa leo hii ukisema unamuondosha mkurugenzi na kuacha walio chini yake ambao kiuhalisia ndio watekelezaji wakuu wa hayo madudu hapo unakuwa umefanya nini?

Hiki kinachofanyika ni sawa na kuzima moto kwa kutumia mabua, kwa juu unaona kama moto umezimika ila chini unafukuta vile vile.
Nani kasema Director ndio alifanya madudu pekee,yeye ndio alitakiwa kuifumua hiyo safu yake ya watumishi na hakufanya hivyo so anawajibishwa yeye.
 
Kuna kundi la matajiri wasiozidi 10 wanaongoza kupitisha bidhaa zao hapo bandarini, wakubwa hao wametajirika kwa miaka mingi kupitia hyo bandari, wanazo pesa za kutosha ambayo wanaweza kumuweka chini mtu yoyote na akalamba asali.

Wakubwa hawa hawa wana connection nzito ndani na nje ya serikali, kama ukitaka kuwazingua sana basi ujiandae kuzinguliwa. Nchi hii ya Tanzania sio rahisi kama watu wanavyofikiria.

Kama ukitaka kudumu sehemu lazima uwe mtu wao, ujue kula nao. Nchi hii inahitaji total reformation, CCM walipoifikisha hii nchi Mungu ndio anajua.
 
Yuko huku!👇👇
Dar es Salaam. Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Madeni Kipande (66) amesomewa mashtaka ya kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh4.2 bilioni akiwa amelazwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI), Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Amesomewa mashtaka akiwa kitandani leo Jumatatu Julai 4, 2022 baada ya kufanyiwa upasuaji wa mgongo katika hospitali hiyo.
Aisee DPP na wenzie hawana huruma
Si wasubiri awe discharged!

Ama inatakiwa kuwa vipi?
 
Bandari bado wahusika wanashindwa kuteua watu educated na experienced na mambo ya bandari. Wapo wasomi wazuri pale DMI wengine mpaka wamestaafu akina Mzee Mayagilo hawa wameanza kwenye Ubahari to Marine engineering to Management PHDs.

Serikali inahitaji kuwekeza kwenye Teknolojia ambayo italeta newly improved controls. Mfano Port of Durban .

Suala la Hamisi kwa uzoefu wangu na hisia ni kwamba alijitahidi kutenda na kujali wafanyakazi lakini pia alikula kwa kamba yake ila kilichomtoa pale ni kwamba kuna matajiri fulani ambao wanafanya shughuli zao za mizigo wameibuka awamu hii ya mama nadhani alishindwa kwenda nao sawa wakaamua wamwage ugali kwa bosi wake. Bandarini kuna matajiri hawa kama hawa wanaofadhili team ya wananchi wale kama hutoweza kwenda nao sawa wanauwezo wa kukujengea fitina ukatolewa wale huwa mazungumzo yao ni magogoni, kwa katibu au kwa mzee wa uongo wakisha kuchongea huko lazima utatolewa tuu.

Nadhani kazi hiyo ingetangazwa na watanzania wenye vigezo wakaiomba. Yupo kijana wa Liundi anapiga sana kazi pale TPA kama Business dev manager sijui au Port manager. Wapo wasomi wamepita DMI wamekaa scandinavia na wamecheza na bandari wanajua nini kifanyike tusione ubaya kuchukua diasporas.
Hatuna proffessionalism.

Siasa zipo kila mahali.

Kila anayewekwa mahali basi ni kwa ajili ya kulinda maslahi flani.

Nani akupe kazi mtu ambaye "hawakufahamu" halafu wakitaka kufanya yao uwakwamishe??

Hapo bandarini patanyooka kama tukipata watu wazalendo , watendaji na wanasiasa ila bila hivyo tutaendelea kufukuza watu kila siku.
 
Watu somo la kula kwa urefu wa kamba wame lielewa na wanapiga kisawasawa.

Kuisaidia bandari lazima issues zote ziwe computerized, hamna watu kutembea na makaratasi.Itasaidia kupunguza japo haitomaliza ufisadi.
 
Back
Top Bottom