Rais Samia atengua uteuzi wa Eric Hamissi, Mkurugenzi Mkuu wa Usimamizi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA)

Mchango wa kwanza kabisa unaofikirisha.

JF nako kumekuwa sehemu ya kushangilia tu, uchambuzi wa kutumia akili umekuwa adimu.

Anayejua sababu za Eric kutumbuliwa, tofauti na haya aliyoeleza hapa mkuu 'Mookiesbad98' ayaweka hapa tuyajadili.
 
Ngoja niotee unazungumzia Gsm, Azim dewji mzee Wa Simba Logistics, TRH , Alistair, Bollore ,FFT, Manji
 
Ikibinafsishwa ndio inakufa kabisa. Rejea kilichowahi kutokea kwenye Reli, Shirika la ndege na viwanda
Kipi bora kati ya shirika kuwa chini ya serikali na kuleta hasara maana serikali inabidi kila mara ilisaidie hilo shirika au kulibinafsisha na kukosa vyote yaani hasara na faida vyote hakuna
 
Kipi bora kati ya shirika kuwa chini ya serikali na kuleta hasara maana serikali inabidi kila mara ilisaidie hilo shirika au kulibinafsisha na kukosa vyote yaani hasara na faida vyote hakuna
Unapozungumzia bandari pia unazungumzia usalama wa nchi.
Hapo ndio karibu vitu vingi hupita, isipokua chini yetu huenda hata na usalama wetu ukawa mdogo. Kwa nchi zetu hizi za ulimwengu wa tatu na aina ya Teknolojia tuliyonayo ni mara mia sehemu Kama hivi kuendelea kuwa chini ya serikali

Kila mara tumeona hata wizara zikiwa hazifanyi vizuri + halmashauri, Ina maana nazo tuziondoe? Sasa tutakua na serikali kweli?
 
Ni topic let's debate, huwezi binafisisha serikali it's impossible, ila sisi wapiga kura nasi tujilaumu maana ndio tunawapigia kura watawala wetu, let's use the power of vote to shake things up, katiba mpya ni jambo jema maana itatuletea judiciary huru na idara zingine, mamlaka yetu ya bandari for now imepata cancer mbaya na imeshaenea mwili mzima, shirika hili lipo ICU now
 
Usalama wa nchi mmmmmm sidhani,Botswana ni land locked country na ipo very stable country labda zaidi yetu
 
Rais Samia tengua pia uteuzi wa Dpp Kweka, tangu umteue ana kazi ya kushinda Moshi na Arusha kutengeneza kesi feki za kumshitaki Sabaya.

Pia meneja wa TRA mkoa wa Kigoma bwana Gabriel Mwangosi amesimamishwa kazi na kamishina mkuu wa TRA bwana Alphayo Kidata baada ya kupandisha ushuru wa forodha mkoani humo kutoka millioni 15 kwa mwezi hadi millioni 300 kwa mwezi!

Alichokifanya bwana Mwangosi alipofika Kigoma ni kuziba mianya yote ya upigaji na kuwaelekeza wafanyabiashara wote kulipa mapato halali TRA na kupata risit halali matokeo yake mapato yakapanda maradufu kitendo ambacho kiliwakera wakubwa ikiwemo wafanyabiashara wakubwa na kuamua kumzushia zengwe na hatimaye amesimamishwa kazi na mapato ya forodha mkoani humo yameshuka tena na kuwa vilevile millioni 15 kwa mwezi!.

Ni kama tu Sabaya alivyoikuta wilaya ya Hai ikiwa ya 144 kwenye mapato na kuipandisha mpaka ikawa ya nne kitaifa lakini akaishia kuzushiwa zengwe na kupelekwa mahakamani. Jambo hilo la wazalendo kutafutwa kwa tochi na kuzushiwa mazengwe limemkera mbunge Tabasamu na kukataa kuomba radhi kwenye mwongozo wa waziri Simbachawene.

 
Kinachofuata ni kukutengenezea wewe,ya uhujumu uchumi ya ukweli kweli ongeza na ya ujambazi
 
Mkuu, naona leo siyo siku nzuri. Kuna kelele nyingi mno.

Ninakubaliana na wewe kuhusu umuhimu wa kulijadili swala hili kwa kina.

Uozo wote tunaouona katika watendaji sehemu mbalimbali ni matokeo ya uongozi mbovvu serikalini. Hii ndiyo dhana yangu kuu katika jambo hili.
Kwa hiyo, kama unataka kurekebisha huko kwingine kote, ni lazima uanze kurekebisha panapoanzia uozo, serikalini.
Na ni kweli, ninakubaliana na wewe, kwamba mwenye mamlaka ya kurekebisha huko serikalini ni mwananchi anayepiga kura kwa kuwachagua kwa uangalifu hawa viongozi wanaounda serikali.

Mtu wa kwanza kabisa ni huyo rais, na wengine wote wanaopigiwa kura, kama wabunge, n.k.

Bado tutajiuliza, je wananchi wanao ufahamu na uwezo wa kufanya kazi hiyo muhimu? Wataacha kuchagua viongozi wao kwa sababu tu wamepewa zawadi ya ubwabwa?

Huenda kutakuwa na siku tytabahatika kulijadili hili kwa utulivu zaidi humu humu JF.
 
Duu!Ndio tumefikia huku kweli? Mtu aliyepandisha mapato kutoka mil.15 kwa mwezi hadi mil. 300 unamsimamishaje kazi? Au labda kuna mambo mengine nyuma ya pazia ambayo wengine hatuyafahamu?
 
Hivi hii tabia mbaya ya kuomba watu wafukuzwe kazi tumeitoa wapi ? Maana mpaka mkazini ipo sana siku hizi ,huku Jamii Forum inaongozwa na kina pascal Mayala .Tutafukuza mpaka watu wa Maana kwa sababu ya Majungu
 
Kwani tanzania wanachi wanachagua au wanachaguliwa? Viongozi wanawekwa tu.
 
Hivi hii tabia mbaya ya kuomba watu wafukuzwe kazi tumeitoa wapi ? Maana mpaka mkazini ipo sana siku hizi ,huku Jamii Forum inaongozwa na kina pascal Mayala .Tutafukuza mpaka watu wa Maana kwa sababu ya Majungu
We huoni Kweka anachofanya?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…