Rais Samia atengua uteuzi wa Eric Hamissi, Mkurugenzi Mkuu wa Usimamizi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA)



Erick ni mpambaji sana , Mungu amtangulie huko aendako
 
Inategemea na vile unavyobinafsisha,wao serikali wanatakiwa kubaki kwenye kusimamia kodi tu,shughuli za kutoa mizigo sekta binafsi wapewe wafanye
Wala hakuna Cha kutegemea, Tanzania ni hii hii ya jana na leo tena Bora ya Jana, ya leo imejaa watu wenye tamaa.
Nakuambia ikibinafsishwa itapewa watu wa viongozi wakubwa huko watachukua kila cent na hakuna mtachowafanya na mwisho itajifia
 
Wazo zuri Ila Nina wasiwasi na huo uthubutu wa kuwapeleka vijana wakajifunze kama utafanyiwa kazi.
Kubinafsisha ni wazo zuri? Ni shirika lipi baada ya kubinafsisha liliendelea kuwepo?
Reli? aTCL, viwanda, TTCL? Hayo ni kwa uchache tu yaliyotokea naamini unakumbuka
 
Ulishawahi kujiuliza kwa nini vyama vya siasa (hususan nchini) vinachipuka kuliko kiwango cha utasibishaji wa bakteria (bacteria binary fission)? Ukipata jibu, umepata! 🙂 🙂 🙂
 
Huyo huenda hayupo TZ.
Hii Tz ukiweka weledi na akili utaibiwa mpaka mwenyewe utakoma
 
Wajenge bandari kubwa ya Bagamoyo,kutumbua na kitumbua hakutaleta ufanisi japo bandarini.
 
Bandari inatakiwa ifumuliwe kuanzia chini kabisa mpaka kileleni. Hii mambo ya kuondoa mtu mmoja mmoja huku kuacha mashina na mizizi ni ujinga tu.
Nashauri isifumuliwe, bali kila kitu kuanzia maji ya bahari, vyombo vya baharini vyote vinavyohusika, miundombinu, vifaa na zana zote za teknolojia na TEKNOHAMA, pamoja na nyaraka zote za serikali na mifumo ya kutunza fedha na fedha yenyewe, vihamishwe hapo, vipelekwe mbali kabisa, hata kule Dodoma ama Morogoro au Singida ndanindani huko.

Hao walevi wa ufisadi waachwe peke yao watapetape kama samaki aliyerukia nje ya dimbwi la maji. Hao manyang'au si watu wazuri kwa usalama wa nchi na maendeleo ya Watanzania.

Kama hamtaki, endeleeni kuwachekea, mtavuna mabua ya kupikia! Kule Uchinani wangechezea kitanzi cha milele.
 
Hivi kipande wa Jakaya yuko wapi
Yuko huku!👇👇
Dar es Salaam. Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Madeni Kipande (66) amesomewa mashtaka ya kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh4.2 bilioni akiwa amelazwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI), Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Amesomewa mashtaka akiwa kitandani leo Jumatatu Julai 4, 2022 baada ya kufanyiwa upasuaji wa mgongo katika hospitali hiyo.
 
au tunashauri iundwe WIZARA maalumu inayo shughulikia BANDARI ZOTE maana naona kama Wizara ya Prof. Mbarawa imeelemewa na kujikuta imejikita kwenye mbarabara zaidi na hivyo Bandari zimeachiwa mchwa wanatafuna.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…