Rais Samia atengua uteuzi wa Eric Hamissi, Mkurugenzi Mkuu wa Usimamizi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA)

Kubinafsisha ni wazo zuri? Ni shirika lipi baada ya kubinafsisha liliendelea kuwepo?
Reli? aTCL, viwanda, TTCL? Hayo ni kwa uchache tu yaliyotokea naamini unakumbuka
Imagine serikali ishindwe, then mtu binafsi kama vile Bakhresa aweze! Hili ni tusi kubwa sana kwa wale wote waliokabidhiwa dhamana ya uongozi wa nchi.
 
Chuma kilikuwa kimeshaanza kupaweka sawa, upuuzi umerudi kwa speed ya 9G...Tukisema acheni Chuma kipumzike mtuelewe.
 
au tunashauri iundwe WIZARA maalumu inayo shughulikia BANDARI ZOTE maana naona kama Wizara ya Prof. Mbarawa imeelemewa na kujikuta imejikita kwenye mbarabara zaidi na hivyo Bandari zimeachiwa mchwa wanatafuna.
Nadhani iitwe Wizara Maalum, kama zilivyo Kanda Maalum za kipolisi.
 
Mzizi wa fitna ni KATIBA mpya.

Timua kikosi KAZI Cha mchongo,

Rudisha mezani Rasimu ya Judge Warioba. Tuanzie hapo Maboresho....
 
Tusisahau Kagame anasema aweza itajirisha Tz nzima kwa kutegemea bandari tu,yaani mengine tupa kule!!
 

Kila wakati huwa nalisema hili field zinatakiwa watu waende
Huwezi kumpa mtu asimamie sehemu ambazo ndio zinaingiza hela ndefu anakuwa ana uzoefu wa kusoma na kufanya kazi hapa hapa au kumtoa kitengo kingine kabisa na kumpa nafasi tu

Hawa wanatakiwa wakaive kwa wale wanaojua kuendesha kazi hizi
 
Iundwe tume na nani?
Waunda tume hao hao mizizi yao imeanzia bandarini😂
Sasa tufanyeje? Waachiwe wale tu, maana hizi tumbua-tumbukiza hazijaonesha matokeo chanya, na muda unaenda.

Afadhali achaguliwe mmoja anayekula kiduchu, abaki hukohuko milele. Because, huku kutumbuliwa nako kunawafanya wakae mguu pande, mguu sawa. Akiipewa nafasi tu, anamega mnofu mkubwa akijua huenda kesho asiwepo.

Kazi kwelikweli! Hivi Elon Musk hajakamilisha mradi wake wa kuhamia Mars?
 
Yes, tukubali tu kwamba tumeshindwa tumpe mwekezaji aendeshe ili sisi atulipe kodi yetu. Kuna muda Kagame aliomba tumpatie ili awe anatupatia kwa mwezi Trillion 1, tukagoma. 🙂
Aisee! Wabunge kwani wanasemaje?
 
Wasipofanya hivyo, kamba iliyowashikilia mkasi unapitishwa, wanadondokea kuzimu. Umeelewa?
 
Kama tatizo ni pesa pale bandari, nashauri mizigo tu ndiyo ishushiwe hapo, pesa zipitishiwe kule Tanga au Bagamoyo. Ila pale Bagamoyo nako zitavukaje kile kiunzi cha Msoga?
 
Tangu lini Wabongo wakaelewa? Lugha pekee wanayoielewa Watanzania (na Waafrika) ni SHURTI! Wanaelewa baada ya kitendo kufanyika.
yule Mzee alikuwa na mapungufu yake ila kwa unyan'gau uliokuwepo pindi anachukua nchi ilitakiwa vile atleast kwa miaka kama 10 hivi then mambo yangekaa sawa tu.... kwa sasa Mapaka yamerudi Shamba la bibi kila kitu ni hovyo,watu wanajipigia vya kutosha, mwananchi mnyonge karudi unyongeni no body care na hakuna kiongozi mkali wa kukemea haya..! kama RAISI ANALALAMIKA, Ni huruma ya Mungu tu tunaisubiria.
 
Ulimi mmoja unavutia Mashariki ya Kati, mwingine ni mrefu ambao shina na mizizi yake iko Magharibi. Mwamba ngoma, huvutia kwake. Ni mwendo wa ^Ukitunyima tonge, tunakulipua!^
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…