Rais Samia atengua uteuzi wa Eric Hamissi, Mkurugenzi Mkuu wa Usimamizi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA)

Rais Samia atengua uteuzi wa Eric Hamissi, Mkurugenzi Mkuu wa Usimamizi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA)

TRA ni kirusi kama virusi wengine
Wanataka kodi kubwa ya kumfilisi mfanyabiashara

Watanzania wanapenda sana kulipa kodi ila kodi ziwe za chini watu wengi wahamasike kulipa tatizo hao wapumbavu wakija kukukadilia kodi utatamani ufunge duka ukalime.

Nyie wenye matumbo ya mbele ebu shusheni kodi watu tulipe kodi.
 
Kuna kundi la matajiri wasiozidi 10 wanaongoza kupitisha bidhaa zao hapo bandarini, wakubwa hao wametajirika kwa miaka mingi kupitia hyo bandari, wanazo pesa za kutosha ambayo wanaweza kumuweka chini mtu yoyote na akalamba asali.

Wakubwa hawa hawa wana connection nzito ndani na nje ya serikali, kama ukitaka kuwazingua sana basi ujiandae kuzinguliwa. Nchi hii ya Tanzania sio rahisi kama watu wanavyofikiria.

Kama ukitaka kudumu sehemu lazima uwe mtu wao, ujue kula nao. Nchi hii inahitaji total reformation, CCM walipoifikisha hii nchi Mungu ndio anajua.
Lakini tumeyapigia kelele haya mambo muda mrefu sasa naona mmeanza kuelewa
 
Matatizo hayako bandarini peke yake.

Matatizo yapo kila mahala, hata kwa wateuzi wenyewe.

Sasa jiulize, hapa katoa usuluhishi gani juu ya tatizo lililopo bandarini.

Huyu bwana mdogo aliyeteuliwa naye siku chache zijazo utasikia kishashindwa kazi.

Mbaya zaidi ni kutochukua muda kufahamu tatizo la sehemu hiyo hasa ni lipi, linalofanya pawe na 'turnover' kubwa kiasi hiki?
Kwani Mama kasema Eric ana tatizo au ameamua kumbadilisha tu na huenda anataka kumpangia kazi nyingine.
 
Ni kweli mkuu, sasa sijui tufanye nini kuondokana na hali hiyo?
Hao wanaokula huko kwenye bandari, madini,n hifadhi kama ngorongoro ndio wanaohakikisha Tanzanua hatupati viongozi tunaowataka bali wanaowataka wao.

Hizo safu za viongozi na management kama hizo za TPA ni watu hatari sana. Hawapo hapo kibahati mbaya.
 
Una hatari na nusu. Sabaya kawa mzalendo!
Rais Samia tengua pia uteuzi wa Dpp Kweka, tangu umteue ana kazi ya kushinda Moshi na Arusha kutengeneza kesi feki za kumshitaki Sabaya.
Pia meneja wa TRA mkoa wa Kigoma bwana Gabriel Mwangosi amesimamishwa kazi na kamishina mkuu wa TRA bwana Alphayo Kidata baada ya kupandisha ushuru wa forodha mkoani humo kutoka millioni 15 kwa mwezi hadi millioni 300 kwa mwezi!

Alichokifanya bwana Mwangosi alipofika Kigoma ni kuziba mianya yote ya upigaji na kuwaelekeza wafanyabiashara wote kulipa mapato halali TRA na kupata risit halali matokeo yake mapato yakapanda maradufu kitendo ambacho kiliwakera wakubwa ikiwemo wafanyabiashara wakubwa na kuamua kumzushia zengwe na hatimaye amesimamishwa kazi na mapato ya forodha mkoani humo yameshuka tena na kuwa vilevile millioni 15 kwa mwezi!.
Ni kama tu Sabaya alivyoikuta wilaya ya Hai ikiwa ya 144 kwenye mapato na kuipandisha mpaka ikawa ya nne kitaifa lakini akaishia kuzushiwa zengwe na kupelekwa mahakamani. Jambo hilo la wazalendo kutafutwa kwa tochi na kuzushiwa mazengwe limemkera mbunge Tabasamu na kukataa kuomba radhi kwenye mwongozo wa waziri Simbachawene.
 
Kashaiba zimemtosha...
Anaenda iba mwingine..
 
Hao uliowataja wanatakiwa wachungunzwe na takukuru, huenda huo unaoita utengenezaji wa case fake unawapatia hela ya sigara mara kwa mara.
 
HUYU DG KAFANYA KAZI SANA KWA MDA MFUPI LAKINI FITINA ZA WAARADU WA SILENT INN NDO ZIMEMUONDOA
 
TRA ni kirusi kama virusi wengine
Wanataka kodi kubwa ya kumfilisi mfanyabiashara

Watanzania wanapenda sana kulipa kodi ila kodi ziwe za chini watu wengi wahamasike kulipa tatizo hao wapumbavu wakija kukukadilia kodi utatamani ufunge duka ukalime.

Nyie wenye matumbo ya mbele ebu shusheni kodi watu tulipe kodi.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] umeongea kwa uchungu sana
 
Yani Serikali inashindwa kuisimamia bandari..
CCM ni laana aisee..
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] umeongea kwa uchungu sana
Mkuu hawa jamaa sio kabisa..
Walikuja kumkadiria mtu hapa alitamani afunfe duka..alichowajibu Mungu tu ndo anajua..

Hawako fea kabisa wanadhani unapata faida kubwa kumbe maisha yetu tunayajua..
 
Ngoja niotee unazungumzia Gsm, Azim dewji mzee Wa Simba Logistics, TRH , Alistair, Bollore ,FFT, Manji
Watu wa ndani wa TPA wanawajua hawa watu, TRA wanawajua hao watu, serikali kuu kupitia vyanzo vyao vinawajua fika. Tatizo ni kua hao ndio wadhamini wa wakubwa na chama chao, walihusika kuiweka madarakani awamu fulani chini ya kikundi chao cha "wanamtandao".

Jamaa fulani alikuja akajitahidi kuwadhibiti, ila walimtangulia.... nchi hii kwenye sekta ya Nishati ya gesi, madini,mafuta, umeme pamoja na rasilimali kama mbuga za wanyama nk ni za wenyewe.

Tumbua huyu weka yule haitatusaidia. Ni lazima kuangalia upya sera za kulinda maeneo ya kimkakati ya nchi. Kwa bandari zilizopp Tanzania ni eneo la kimkakati tulilopo ilitakiwa tuwe mbali kiuchumi, sisi sio wa kukopa trilion moja kujenga madarasa.
 
Usalama wa nchi mmmmmm sidhani,Botswana ni land locked country na ipo very stable country labda zaidi yetu
Umenielewa kweli? Ni sawa na kusema mipaka ya haao Botswana iwe chini ya private companies.
 
Back
Top Bottom