Rais Samia atengua uteuzi wa Pauline Gekul saa chache baada ya kutuhumiwa kufanya unyanyasaji kwa mtoto

Rais Samia atengua uteuzi wa Pauline Gekul saa chache baada ya kutuhumiwa kufanya unyanyasaji kwa mtoto

Hongereni wananchi wa Babati.

Haki imeshinda,Umoja wenu ndiyo ulinzi wenu sasa mtuhumiwa wetu yupo katika mikono salama ya Jeshi la Polisi Tz.

Jaribio lake la Kutoroka mkono wa sheria limezimwa na Wananchi na sasa Polisi wamemtia mbaroni mualifu wetu.

Sasa anachukuliwa MAELEZO YA ONYO katika Ofisi za RCO,Manyara

Pauline Gekul alipanga kutokea Nairobi,Kenya [emoji1139] leo alfajiri baada ya jana Gekul kupata taarifa za kutaka
1.kushtakiwa na 2.Kufukuzwa uanachama wa CCM Wilayani Babati.

Umoja mlio onyesha wananchi wa Babati usiishie hapo tu.

Jutitokeze Kwa wingi Mahakamani ili haki iweze Kuonekana ikitendeka.

Najua Babati inafuraha kama imepata uhuru tangu Jana,lakini tuendelee na kazi ya doria.

Ukatili na ualifu dhidi ya utu unapaswa Kupingwa na dini zote,Itikadi zote na jamii yote mahala popote.

View attachment 2826267

Sent using Jamii Forums mobile app
* Laana ya Chadema inamtafuna.*
 
Hawezi kufanya hivyo kwa Sasa kwa kuogopa jinai.Huyu ni mmoja wa wanawake katili sana na mjinga fulani hivi,limbukeni wa mambo ya mjini mjini.Unaona hata mdogo wake anamfokea yule mama wakati anajua kabisa uwanja umeshachafuka wala hakuwa na tahadhali yeyote kukwepa kurekodiwa.Ushamba ni mzigo na fedheha kwa jamii.Kilichomponza hiyo chalii ni ushamba.Alipaswa akutane na mwendazake Dangote aliyezikwa juzi usiku angemfundisha adabu.
Nilimshangaa jamaa anatukana alafu anamwambia mama nenda kashitaki,nitakukata shingo e..h.kumbe Kuna watu wanajiamini cku hz.yan hakuwaza anarekodiwa?
 
Ikiwa ni mtu Muungwana Mhe Gekul angetoka hadharani kisha akamuomba Hashim na Umma Kwa ujumla msamaha Kwa udhalilishaji aliofanya. Nasi kama sehemu ya Jamii tutamuelewa.

Kuendelea kushupaza komwe kutamgharimu kisiasa na kijamii
Kabla hajaomba msamaha, akamtibu Hashim mpaka apone. Baada ya hapo, amtafutie watataalam wa saikolojia kwa ajili ya kumuweka sawa (Hashim), kwani kitendo alichofanyiwa ni wazi kimemuathiri kisaikolojia, na huenda asilisahau tukio hili mpaka mwisho wa maisha yake yaliyobaki hapa duniani.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria, Mhe. Pauline Philipo Gekul.

View attachment 2824966

Saa chache zilizopita, Pauline Gekul ambaye ni Mbunge wa Babati Mjini alituhumiwa kumfanyia unyanyasaji mfanyakazi wake ambapo inadaiwa akishirikiana na watu wengine walimdhuru mwili na kumuingiza chupa sehemu ya haja kubwa.


Hata hivyo, Mbunge Pauline kupitia Katibu wake alikanusha taarifa hiyo katika ujumbe uliowekwa kwenye mitandao ya kijamii ukimtuhumu Hashimu kufanya udanganyifu na kushirikiana na washindani wa Pauline wa kibiashara kumfanyia ushirikina na baadaye ujumbe huo kufutwa kwa maelezo kuwa suala hilo liko mikononi mwa Polisi.

Tukio hili nalo pia ni la kiutengeneza kwa makusudi, na linafanana na lile lililopita siku za nyuma la aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya, aliyewahi kufanya maigizo ya kuyaigiza “Macho ya Nchi” kwenye siku ya Sikukuu ya Wanawake Duniani
 
Back
Top Bottom