Rais Samia atengua uteuzi wa Pauline Gekul saa chache baada ya kutuhumiwa kufanya unyanyasaji kwa mtoto

* Laana ya Chadema inamtafuna.*
 
Nilimshangaa jamaa anatukana alafu anamwambia mama nenda kashitaki,nitakukata shingo e..h.kumbe Kuna watu wanajiamini cku hz.yan hakuwaza anarekodiwa?
 
Ikiwa ni mtu Muungwana Mhe Gekul angetoka hadharani kisha akamuomba Hashim na Umma Kwa ujumla msamaha Kwa udhalilishaji aliofanya. Nasi kama sehemu ya Jamii tutamuelewa.

Kuendelea kushupaza komwe kutamgharimu kisiasa na kijamii
Kabla hajaomba msamaha, akamtibu Hashim mpaka apone. Baada ya hapo, amtafutie watataalam wa saikolojia kwa ajili ya kumuweka sawa (Hashim), kwani kitendo alichofanyiwa ni wazi kimemuathiri kisaikolojia, na huenda asilisahau tukio hili mpaka mwisho wa maisha yake yaliyobaki hapa duniani.
 
Tukio hili nalo pia ni la kiutengeneza kwa makusudi, na linafanana na lile lililopita siku za nyuma la aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya, aliyewahi kufanya maigizo ya kuyaigiza “Macho ya Nchi” kwenye siku ya Sikukuu ya Wanawake Duniani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…