Rais Samia atoa pole kufuatia kifo cha Benedicto Mallaba aliyekuwa Jaji wa Mahakama Kuu

Rais Samia atoa pole kufuatia kifo cha Benedicto Mallaba aliyekuwa Jaji wa Mahakama Kuu

Sijapewa username bado

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,775
Reaction score
2,891
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametoa salamu za pole kufuatia kifo cha Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu Benedicto mallaba kilichotokea Disemba 19, 2025.

===
Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaungana na Watanzania wote kutoa salamu za pole kufuatia kifo cha Julius Benedicto Mallaba aliyekuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania. Bwana alitoa, na Bwana ametwaa; jina la Bwana na libarikiwe.
Ikulu Mawasiliano/ikulu_mawasiliano/ikulu Tanzania Ikulu Tanzania/Ikulumawasiliano/Ikulu Tanzania/Ikulu Tanzania
SaveClip.App_604209440_18306885529258462_6190560366216873924_n.jpg

===

Taarifa ya kifo chake kama ilivyotolewa na Mahakama ya Tanzania

Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Julius Benedicto Mallaba enzi za uhai wake.

Mahakama ya Tanzania inasikitika kutangaza kifo cha Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Julius Benedicto Mallaba kilichotokea leo tarehe 19 Desemba, 2025, saa 10 alfajiri, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu kwa ugonjwa wa sukari na shinikizo la damu.

Marehemu Jaji Mallaba alizaliwa tarehe 12 Machi, 1960. Aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania tarehe 25 Julai, 2015 na kustaafu rasmi mnamo tarehe 12 Machi, 2020.

Kwa Mujibu wa Msemaji wa Familia, msiba upo nyumbani kwake Mbweni jijini Dar es Salaam. Taratibu nyingine za mazishi zitatolewa na Familia.

Mahakama ya Tanzania inaungana na ndugu, jamaa na marafiki kuomboleza msiba huu wa kuondokewa na mpendwa wetu.

BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.
1766396338647.png
 
Kuzaliwa 1960 kustaafu 2020? Jaji?

Kwa ugonjwa? Kustaafishwa? Kuna kitu hakipo sawa...
 
Back
Top Bottom