Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa tahadhari kwa wana CCM kuhusu matumizi ya akili Mnemba, akisema kuwa inaweza kutumika vyema au kutumika vibaya kueneza uzushi na Uchochezi.
Dkt. Samia ameyasema hayo alipokua anazungumza na Wajumbe wa Mkutano wa CCM Taifa kabla ya kufunga mkutano huo tarehe 19 Januari, 2025 katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Convetion Centre Dodoma.