Rais Samia awaagiza Wizara ya Utamaduni kuwafundisha vijana mila na desturi kupitia michezo ya UMISSETA na UMITASHUMTA

Rais Samia awaagiza Wizara ya Utamaduni kuwafundisha vijana mila na desturi kupitia michezo ya UMISSETA na UMITASHUMTA

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760

Rais Samia ameilekeza wizara ya utamaduni, sana ana michezo kukamilisha mwongozo wa utambuzi wa machifu na viongozi wa kimila katika wilaya na mikoa utakaoainisha majukumu yao yao ya kimila na kijadi.

Rais Samia ametoa maelekzo hay oleo wakati akizungumza na viongozi wa kimila na machifu kutoka Tanzania nzima kwenye hafla iliyofanyika Ikulu, Chamwino Julai 20, 2024.

Rais Samia amesema viongozi wa kimila na machifu wana mchango mkubwa katika kulinda maadili na kutatua changamoto za kimaadili katika jamii licha ya kuwa yanashughulikiwa katika ngazi ya serikali.

Pia ametoa rai kwa mchifu kote nchini kuendelea kujenda mvuto na uaminifu wa watu ili waweze kutoa mchango wao ipasavyo kwa ushirikiano na serikali katika utatuzi wa migogoro inayoikabili jamii.

Vile vile Rais Samia amekea vitendo vya utekaji na mauaji ya watoto kwa Imani potofu za ushirikina ambavyo ni kinyume cha maadili ya Watanzania na kuwasihi Machifu na wananchi wote kukemea vitendo hivyo.

Rais Samia pia ameitaka Wizara ya Utamaduni kuimarisha michezo ya Umoja wa Michezo ya Shule za Msingi na Sekondari (UMISSETA na UMITASHUMTA) ikiwa ni sehemu ya kuwafundisha na kudumisha mila na desturi zetu.
 
Back
Top Bottom