Rais Samia awabadili Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa Diwani Athuman na Katibu Mkuu Kiongozi Hussein Kattanga

Ni jeshi ila ambalo utendaji wa kazi zake unategemea raia kwa kiwango cha juu sana kuliko majeshi mengine yote yaliyopo Tanzania
nilitaka nimuelekeze huyo jamaa apo juu kua tiss ni jeshi rasmi kati ya majeshi ya nchi hii.
 
Kivipi sio demotion, wakati Katibu Mkuu Kiongozi ni Mtumushi wa juu kabisa katika utumishi wa umma na anaripoti kwa Rais, wakati hivi sasa atakuwa anaripoti kwa Katibu Mkuu-Wizara ya Mambo ya nje!!!
hayo mambo ni mtambuka sana mkuu,inawezekana akawa ana report moja kwa moja kwa rais vivo hivyo
 
Habari wakuu. Nawapongeza viongozi wote walioteuliwa. Je kuna yeyote anayeweza kutupatia umri wa hao wateule. Kuna dot nataka kuziunganisha hapa.
Ahsante
 
Mkurugenzi mpya yuko pisi sana.
Naomba niishie hapo
 
Mabadiliko yanalenga kuongeza kasi zaidi kwenye maendeleo ya nchi yetu.

ni mabadiliko yenye nia njema ya kujenga sio kukomoa wala kubomoa.
Kama tukiona maisha mtaani yameboreka,tutajua kwamba kweli mabiliko haya yalikuwa na nia hiyo,otherwise huu utabaki kuwa usanii.
 
Yamekuwa hayo tena?.

Mbona hata Samia mwenyewe anazichota tu pale Ikulu.

Sema kuna mafaili tu hayasogei pale, mama anatakuwa hayatoi kwa sababu pengine yanagusa watu wake na ndio maana Sasa jamaa anaondolewa ili wabaki wenyewe.
Huyo mjomba wako ni choli tangu akiwa mkurugenzi wa manispaa ya kinondoni hana usafi wowote pia uraia wake una utata
 
Hajafanya kitu kama hajachangua Wizara ya Fedha. Hii ndiyo inaangusha Tanzania kwa sasa.
 
Mkurugenzi mpya yuko pisi sana.
Naomba niishie hapo
Siku zote zinapokuja sura mpya katika teuzi mtatoa kila aina ya sifa kuwa huyu ni jembe, pisi sana, mtu wa watu, kichwa, ana aleji na rushwa, hana ubaguzi, msikivu, mtu wa haki, na sifa zingine ambazo mwanadamu hana lakini mtampatia tu kuwa akikuangalia tu anaweza kugundua mke wa mtu uliyetembea naye.

Then baada ya miaka miwili mitatu akitolewa mnaanza tena kusema " kwanza nashangaa ilikuaje mtu kama huyu kupewa nafasi nyeti kama hii,
 
 
Hakuna lolote hapo ni udini.sasa ndio mabadiliko hayo,eti kuongeza uwajibikaji endelea tu mama watu wanakuzoom vzr tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…