Rais Samia Suluhu Hassan ameonya Wanasiasa, hususani wabunge na Madiwani kuanzisha vijiji katika maeneo ya hifadhi pindi wanapoona chaguzi zinakaribia na hawakubaliki.Rais Samia amesema hayo leo Jumatatu Agosti 5, 2024 katika mkutano wa hadhara alipozungumza na wananchi wa Ifakara katika Uwanja wa CCM Ifakara mkoani Morogoro, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya siku sita mkoani humo.
Unajua zipokaribia chaguzi hizi hasa Madiwani, Mtu akiona yuko vibaya kwa upande mwingine wa eneo lake anakwenda kusogeza watu kuanzisha kijiji, sasa haya ya kuanzisha vijiji bila kujali tunavianzisha maeneo gani, vijiji vingi vilivyoanzishwa ndani ya maeneo ya hifadhi ni kwa ajili ya Wanasiasa.
Soma pia: Rais Samia: Baadhi ya Madiwani wanahusika katika kusababisha Migogoro ya Ardhi