Ojuolegbha
JF-Expert Member
- Sep 6, 2020
- 1,278
- 797
Nawatakia kila la kheri wanafunzi 1,230,780 wa Darasa la Saba mlioanza Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi leo. Mnatoka hatua moja ya elimu na malezi kwenda nyingine katika safari yenu ya kujiandaa kutoa mchango wenu wa maendeleo kwa Taifa letu. Serikali imeandaa mazingira sahihi ili muweze kufikia lengo hili.
Ahadi yangu kwenu katika safari yenu ya elimu na maisha ambayo tayari inatekelezwa ni; nafasi katika shule kwa kila atakayefaulu kuingia Kidato cha Kwanza 2025, miaka minne ya sekondari ya awali bila ada, miaka miwili ya Kidato cha Tano na Sita bila ada, Chuo cha Ufundi katika kila Wilaya kwa mtakaochagua njia hii na mikopo ya Elimu ya Juu kwa mtakaofaulu kwenda Vyuo Vikuu.
Kazi hii inakwenda sambamba na kuendelea kuboresha sera za uchumi wetu ili uweze kuzalisha fursa zaidi kwa kila mmoja wenu kadiri mnavyoendelea kukua na kuingia katika nguvu kazi.
Mwenyezi Mungu awaongoze.