Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Rais Samia akiweka Jiwe la Msingi Upanuzi wa Msikiti Mkuu wa Ijumaa Tanga Februari 26, 2025
"Mmenipa heshima kubwa sana kuja kuweka jiwe la Msingi katika Msikiti huu wenye historia kubwa na ya muda mrefu hapa Tanga na Afrika Mashariki kwa ujumla"
"Niwashukuru sana kwa maneno mazuri mliyoyasema juu ya serikali yenu na kwa dua mliyoniombea leo, ambazo mlikuwa mkiniombea na mkituombea mara kwa mara sisi viongozi na Taifa kwa ujumla, mimi ninaamini kwa dhati ya moyo wangu kwamba dua zenu njema viongozi wa dini na waumini wote pamoja na juhudi zetu Serikali, zinatusaidia sana kuendelea kutuweka pamoja kama Taifa"
"Ni shukrani maalumu kwa wenzetu wa Lake Group kwa kujitolea kuweka nguvu zao katika ujenzi wa Msikiti ambao nimeuwekea jiwe la msingi"
"Tuna mipango mikubwa sana kwa Mkoa wa Tanga, lakini kama mipango hiyo itakuta vijana wameshaathirika na dawa za kulevya, haitakuwa na maana. Tuendelee kushirikiana na Serikali kupambana na biashara hii haramu inayowaathiri vijana wetu."