Wakuu tufuatilie hii ni Mubashara
Leo Rais Samia atashiriki kuzindua Bandari Kavu ya Kwala, mradi unaotarajiwa kuboresha usafirishaji na kupunguza changamoto ya Foleni hususani Kwa magari makubwa (Malori)
Soma pia: Julai 31, Rais Samia kuzindua bandari kavu ya Kwala, malori kuingia mjini sasa basi
Rais Samia amezindua Treni ya kusafirisha Mizigo SGR iliyopo pwani Kwala pia ameweka jiwe la Msingi Kongani la Viwanda Kwala, Pwani
Baada ya hapo Rais Samia anatarajiwa kufika eneo la Bandari kavu kisha kuelekea eneo maalum lililoandaliwa kwa ajili ya Mkutano.
Rais Samia amewasili katika Bandari Kavu ya Kwala akipewa maelekezo ya mradi huo na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Bandari TPA Plasduce Mkeli Mbossa
Lengo kubwa la Mradi huo ni;

- kupunguza muda na gharama za usafirishaji kwa wafanyabiashara
- Kupunguza Msongamano wa magari katika Jiji la Dar es Salaam
- Kuchochea upatikanaji wa ajira kwa wakazi wa Kibaha na maeneo ya Dar es Salaam na nchini kote kwa ujumla
- Kuchochea uwanzishwaji wa viwanda na uwekezaji kwenye ukanda wa kwala
- Kuongeza mapato ya serikali kutokana na huduma za bandari
- Uzinduzi rasmi wa safari za mizigo za reli ya SGR
- Uzinduzi wa kituo cha kimataifa Logistic cha Kwala
- Uwekaji wa jiwe la Msingi Kongani la Viwanda Kwala, Pwani