Rais Samia azindua jengo la Halmashauri ya Handeni

Rais Samia azindua jengo la Halmashauri ya Handeni

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Jumanne Februari 25, 2025 ,amezindua rasmi Jengo la Halmashauri ya Mji wa Handeni huku akisisitiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma kote nchini.

Rais Samia amewataka watumishi wa halmashauri kuzingatia majukumu yao na kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wananchi bila kujiona kuwa juu yao.

"Yale makoti mtakayovaa na mabrificase mtakayobeba yasiwapandishe mabega. Nyinyi ni watumishi wa wananchi hawa," alisisitiza.Jengo hilo ni mojawapo ya majengo 122 yaliyojengwa ndani ya miaka minne, ikiwa ni juhudi za serikali kuhakikisha huduma zote zinapatikana ndani ya kituo kimoja, kuondoa usumbufu kwa wananchi.


"Tunafanya hivi ili watumishi wawe na sehemu bora za kufanyia kazi na wananchi wapate huduma kwa urahisi," alisema Rais Samia.Rais Samia pia amesisitiza umuhimu wa ulipaji kodi ili kufanikisha maendeleo ya nchi.


Rais Samia pia amesisitiza umuhimu wa ulipaji kodi ili kufanikisha maendeleo ya nchi.

"Miradi yote tunayotekeleza, iwe ni barabara, vituo vya afya, hospitali, au miradi mingine inatokana na kodi zenu. Tunalinda haki ya kila mwananchi kulipa kodi stahiki bila kubambikiziwa, lakini pia msidhulumu kodi za serikali," alisema.

Ameongeza kwa kusema, kuwa serikali itaendelea kuimarisha mifumo ya ukusanyaji wa mapato na kudhibiti mianya ya upotevu wa fedha.

“Kodi ni kwa manufaa yetu, tozo ni kwa manufaa yetu. Tunapokusanya kodi kwa uadilifu, tunaweza kuleta maendeleo makubwa zaidi kwa wananchi,” alisisitiza.


 
Back
Top Bottom