Rais Samia: Bado kuna Wakuu wa Mikoa na Wilaya wanatumia vibaya madaraka yao

Hilo tunalijua atuambie kafanya nini kuhusu hilo. Yeye ndiye anawateua, kwanini asiwatumbue?
 
Hii Nchi ni ya kusadilika
Jana nimeona clip ya Mh Jerr Silaa humu akipinga amri ya Mahakama halali kule Mapinga ya mama Mjane heka zake 12 kuvamwiwa na kujengea
Waziri anaelekeza alipwe kwa bei ya itakayo amuliwa tofauti na Mahakama ilivyo elekeza

Huyu Waziri mbona hakumuachia Mzee Mushi awalipe alio wapora kwa bei hiyo elekezi?

Amuache na Msami alipe kwa bei elekezi

Waziri kajipanga Tena
 
Anaye kwenda kinyume na walaka huo atumbuliwe tu
 

Hilo tunalijua atuambie kafanya nini kuhusu hilo. Yeye ndiye anawateua, kwanini asiwatumbue?
Yule wa Arusha kuna mama mmoja alikuwa akimlilia "baba nisaidie" maana mjukuu wake alibakwa, lakini Mahakama ya Wilaya ilimpa ushindi mtuhumiwa na kuachiwa huru. "Na ikasema rufaa iko wazi." Yet, huyo mkuu baada ya kusikiliza upande mmoja wa huyo mama, alitoa agizo kwa OCD mtuhumiwa akamatwe na kwamba "kesi inaanza upya" na watu kama kawaida yao wakashangilia. Sasa sijui kesi itaanzaje upya na kwa utaratibu gani wakati mahakama ilishasema rufaa iko wazi? Kwa upande wangu, huyo mtuhumiwa hapa ana haki ya kufungua kesi dhidi ya huyo mkuu "for unlawful incarceration" na hii inge'set' precedence kwa viongozi wengine wanaoamua mambo 'arbirarily' bila kufuata sheria. Lakini kwa vile watu wengi hawajui sheria na kwa vile wengine wanakimbilia kuwaogopesha wenzao "usishindane na serikali", watu wengi hukaa kimya na kuumia ndani ndani bila kudai haki zao.
 
kahaba haupigwi vita kwa kukamata. Hii inaonyesha polisi na watawala hawana kazi ya kufanya na wanakumbilia kufanya usanii. Hili unalosema la wapenzi kuvunjiwa faragha yao ni moja tu ya matokeo ya usanii unapongeza! Pole sana kwa kuwa na akili za kutoona uhusiano wa haya mawili.
 
No zitangazwe watu waombe na usaili ufanyike
Ni kweli hizi title za mkuu wa mkoa/ wilaya ni siasa tupu and waste of time and money, ni nafasi za kupeana asante na zinawakilisha favoritism, hizo nafasi ziwe zinawajibika moja kwa moja kwa wananchi, hiring and firing power wapewe wananchi kwa mechanism inayoeleweka , kuna namna nyingi ya kuondoa siasa siasa kwenye hizi title lakini hawataki
 
Video ingetosha kuliko kutuumiza macho na nukuu hii.
 
Yaani yule Nawanda ndio kavunja rekodi, hadi kulawiti, alilewa madaraka sana
 
Hapo ujue fika kwamba mazaa katema cheche. Kwa walengwa: Mwenye masikio na asikie.
 
Mi huwa wanajiuliza waliotunga hii katiba walikuwa ni wazima kichwani?
 
Yule Mkuu Wa Wilaya Aliyetunisha Misuli Kwenye Semina Kuwa Atafanya Lolote Maana Anamwakilisha Rais Kwenye Eneo Lake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…