DOKEZO Rais Samia, Barabara ya Ngorongoro Crater ni mbovu, Watalii wanapata ajali mara kwa mara

DOKEZO Rais Samia, Barabara ya Ngorongoro Crater ni mbovu, Watalii wanapata ajali mara kwa mara

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Hata kama nature ina hatarisha uhai wa watu??
Wewe ni dereva wa hovyo yaani sisi ile kona tunapita na Lori tipper imejaa kifusi zaidi ya 18tonnes na hatuchekechi,yaan cruiser ishindwe kumaliza kona?Ebu fatilia aina ya dereva wanaosabisha ajali eneo lote hifadhi;Wengi ni madereva wasiokuwa na uzoefu wa eneo husika wengi wao upewa kazi za muda na wenye makampuni hasa kipindi cha high season ambapo madereva wazoevu ni adimu hasa ukanda wa kaskazini,so kinachofanyika matajiri wapo tayari achukue dereva yeyote mtaani ilimradi anajua lugha mojawapo ya kigeni ya kuzungia na driving ya mtaani ilimradi hasikose pesa ya wageni.Hawa ndo wale uwa tunawakuta wanachekecha kwenye hiyo kona kali wakti kona hiyo tunapita na malori makubwa bila hata kugusa ukuta,
 
Waweke mtu maalumu akae pale awe anachekecha
 
Waweke mtu maalumu akae pale awe anachekecha
Sema kuna madogo uwa wanajielewa sana akiona mambo yanakuwa magumu uomba msaada getini anawadanganya wageni kuwa kule crater anaetakiwa kuendesha ni guide wa Ncaa, hivyo akifika ofisi ya zamani anajieleza hali yake ya driving kuwa hajawahi kushuka crater wa kupanda ila hataki wageni wajue hilo kulinda kibarua so anaomba msaada wa kupewa dereva kurescue hali tena bure labda akiamua asante.So kwa madogo wenye akili nyingi utumia njia hii,so kwa mara ya anajifunza kushuka na kupanda yeye akiwa kushoto na kazi inaendelea bila hata kuharibika na wageni bila kusanuka au boss wake kujua.But wale wajuaji ndo wote hao waleta balaa.Make ile kona ni kali kwa mtu akiiona ghafla hii hapa na ukuta huu ghafla anachanganyikiwa na kuingia mtero.Wakati kona hiyo eneo kubwa lilopanuka kushoto ili kuitafutia angle ya ukuta inabidi uibie kushoto kidogo huko umeweka 4WD kuanzia chini na hapo unapita na mbili yako taratibu bila kuchekecha wala ngao kugusa ukuta.
NCAA ina watumishi wana roho hakuna mtu anaeweza kukunyima huduma hii ya kukusaidia kupanda na kushuka huku akikufundisha ili next term ujitegemee ukiwa mwenyewe.Sema ma guides mmelishwa matango pori juu ya watumishi wa mamlaka mnawachukia bure mwisho mnashindwa kuwaomba msaada ambao ni haki yenu,badilikeni jamani tukuze utalii wote
 
Rais Samia

Pole na Majukumu ya Kuliongoza taifa.

Kwa niaba ya madereva Guide wa Utalii nipende kuelezea kero juu ya kona kali ya perving ya kupandia kutoka ndani ya Crater.

Mh Rais ni kwamba Mamlaka ya Ngorongoro imeshindwa kuchonga Mwamba hata mita mbili ili kuondoa wimbi la ajali inayotokea mara kwa mara.

Eneo hilo ni hatari na magari mengi hushindwa kuimaliza kona hiyo kwa kuwa ni Landcruiser warbus na pale unaporudi nyuma kuna hatari kubwa kwa kuwa ni shimo na hata wameshindwa kuweka vyuma pembezoni ili kuzuia ajali.

Wakati mwingine wageni huangua kilio pindi gari inaposhindwa kumaliza na kurudi nyuma

Rais Samia ikiwezekani turuhusiwe sisi tunaopita katika eneo hilo tuchonge kwa shoka kwani Adha imekuwa kubwa na wageni wanalalamika.

Rais Samia kero hii mara kadhaa tumekuwa tukiielezea NCAA ila hakuna hatua yoyote inayochukuliwa na hivi karibuni kuna ajali kadhaa zimetokea katika eneo hilo la mlima mkali na kona kali.

Natanguliza Shukrani za dhati

N.B
Niipongeze mamlaka kwa ufuatiliaji wa mara kwa mara wa Barabara zake ambazo ni bora..ila tatizo letu ni Kona ya kubusu wakati unapanda toka Crater
 
Attachments

  • 4404A3B9-98FE-4965-90DE-5A96338B4ADB.jpeg
    4404A3B9-98FE-4965-90DE-5A96338B4ADB.jpeg
    68.7 KB · Views: 6
Wakuu hii kitu izingatiwe kuwa tulilia na Serikali na barabara nyingi ktk hifadhi na hasa Ngorongoro Crater zimefanyiwa maboresho Makubwa.
Hongera Mamlaka ya NCAA kwa kusikiliza Kilio Chetu wadau wa Sekta ya Utalii.
Mama anaupiga mwingi.
 
Kumbe huwa tunalishwa matango wanaposema Utalii unalipa, sasa hata barabara wanashindwa kutengeneza halafu kila siku wanachukua $$$$ zinaishia mifukoni ama
 
Back
Top Bottom