- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Wakuu habari,
Msaada wa uhakika wa hii taarifa kabla hatujaanza kumkaanga Kizimkazi hapa
Msaada wa uhakika wa hii taarifa kabla hatujaanza kumkaanga Kizimkazi hapa
- Tunachokijua
- Baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii walichapisha taarifa iliyoambatana na grafiki mbalimbali zikiwa na ujumbe unaodaiwa kuwa umetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan. Ujumbe huo unasomeka;
"Dharau mnayonionesha hata mwanangu hajawahi kunionesha"
Uhalisia wa madai hayo
Ufuatiliaji wa JamiiCheck kwa kutumia nyenzo za kidigitali umebaini kuwa taarifa hiyo si ya kweli.
Kupitia utafutaji wa maneno muhimu imebainika kuwa hakuna uthibitisho unaobainisha kuwa Rais Samia alishawahi kutoa ujube huo kupitia vyombo vya habari ama mitandao yake ya kijamii.
JamiiCheck imefuatilia kurasa rasmi za mitandao ya kijamii ya Rais Samia akiwemo wa X zamani Twitter na kubaini kuwa hakuna pia ujumbe huo licha ya kuwa pia haupo katika kurasa rasmi za Ikulu am ahotuba zake alizowahi kufanya na kuchapishwa katika Chaneli ya Ikulu Tanzania.