Rais Samia, fanya mabadiliko ya wasaidizi wako hasa Kwenye hotuba; unaweza ukawa na wasomi ila siyo wataalam wala wazoefu

27 October 2021

SEKTA MBALIMBALI ZASHAURIWA KUJIPANGA KUKABILIANA NA UPUNGUFU WA MVUA UNAOTARAJIWA KUTOKEA



Dar es Salaam, Tarehe 27/10/2021
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania imetoa rasmi utabiri wa mvua za msimu kwa maeneo yanayopata mvua za msimu mara moja kwa mwaka, ikijumuisha mikoa iliyopo magharibi mwa nchi ( Kigoma, Tabora na Katavi), nyanda za juu kusini magharibi (Rukwa, Mbeya, Songwe, Njombe, Iringa), katikati mwa nchi (Dodoma na Singida), pwani ya kusini (Lindi na Mtwara), mkoa wa Ruvuma pamoja na maeneo yaliyoko kusini mwa mkoa wa Morogoro katika kipindi cha miezi ya Novemba, 2021 hadi Aprili, 2022.

Akiwasilisha utabiri huo kwa waandishi wa habari, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ambaye pia ni Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) Dkt. Agnes Kijazi alisema kuwa, utabiri huo wa mvua za msimu unatarajiwa kuwa wa wastani hadi chini ya wastani hivyo kuwataka wadau kutoka sekta mbalimbali kuzitumia taarifa hizi za hali ya hewa kwa kujipanga ili kukabiliana na matarajio hayo.

Mkurugezi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa “Natoa ushauri kwa wadau wa sekta mbalimbali wanaotumia taarifa za hali ya hewa katika utekelezaji wa majukumu yao kama vile kilimo na usalama wa chakula, mifugo na uvuvi, maliasili, wanyamapori na utalii, nishati na maji, usafirishaji (nchi kavu, kwenye maji na angani), mamlaka za miji, afya, sekta binafsi pamoja na menejimenti za maafa kujipanga na kutumia njia ambazo zitaweza kukabiliana na upungufu wa mvua unaotarajiwa kujitokeza katika kipindi cha mwezi Novemba, 2021 hadi Aprili, 2022” alisema Dkt. Kijazi.

Dkt. Agnes Kijazi aliongezea kusema, mvua hizo zinatarajiwa kuanza kwa maeneo mengi katika wiki ya tatu ya mwezi Novemba, 2021 na kuisha katikati ya wiki ya pili na ya tatu ya mwezi Aprili, 2022. Hata hivyo, ongezeko kidogo la mvua linatarajiwa mwezi Machi, 2022 katika nusu ya pili ya msimu huo.

Aidha, Dkt. Kijazi alisisitiza kuwa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania itaendelea kufuatilia mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa na kutoa mirejesho ya mwelekeo wa mvua nchini kadri inavyohitajika na kuwashauri wadau kuendelea kuwasiliana na Mamlaka ili kupata taarifa mahsusi za utabiri wa msimu ili kukidhi mahitaji maalum katika sekta zao.

b) Athari na ushauri
(i)Upungufu mkubwa wa unyevunyevu katika udongo unatarajiwa kujitokeza katika maeneo mengi yanayopata mvua za Msimu na kuathiri ukuaji wa mazao.

(ii)Kina cha maji katika mito, mabwawa na hifadhi ya maji ardhini kinatarajiwa kupungua hususan katika maeneo yanayotarajiwa kupata mvua za chini ya wastani.

(iii)Mlipuko wa magojwa unatarajiwa kujitokeza kutokana na upungufu wa upatikanaji wa maji safi na salama.

Kwa maelezo kamili kuhusu utabiri huu tembelea: https://www.meteo.go.tz/publications/single/

Source : TMAonline TV
 
Nimefuatilia hotuba za Rais Samia kwa wakati wote

Amekuwa akifafanua mambo makubwa na mazuri lakini naona kuna upungufu kwenye Pitching ambayo ndio hasa jamii inahitaji kusikia. Katie holiday naungana na dadangu Beatrice kukazia.

Wataalamu wa uandishi na habari cc Pascal Mayala anaweza kuwa umenielewa vizuri

Hotuba zina mambo mengi ila jambo kubwa moja ni muhimu na linabeba Message mahususi ya hotuba nzima na ina brand taasisi ya Rais.

Mfano heading za kesho zitakuwa ni nini ..?

Hakuna heading inayowagusa watanzania sasa sijui tatizo ni wataalamu au nini mbona wapo wajuvi wa siasa propaganda na saikolojia ya jamii waliobobea kwenye uandishi wa habari na mawasiliano.

Nazani hotuba hazivikii Pitching kwa wananchi wa kawaida. Ni hotuba zinazoeleweka zaidi kwa watu wenye uelewa wa wastani sasa huku vijijini watu wahitaji kusikia kuhusu mambo yanayowahusu hasa yale ya chini kabisa kulingana na kuelewa wao.

Please kurugenzi ya mawasiliano ikulu fanyeni kazi yenu
Hamko hapo kutembelea mavieite mko hapo kufanya kazi hasa ya kumsaidia Rais

Nawatakia Mafanikio Makubwa mwaka 2022

Rais Samia
#KAZI IENDELEE
 
Pasco hapa ndio pa kwenda kwa mganga na kuroga. Hii nafasi inamfaa.
 
Pitching, pitching, pitching!
Wewe mwenyewe hata hiyo pitching huwezi kuielezea vizuri.
Hotuba ya mama SSH mbona iko poa tu! Labda utakuwa na matatizo yako binafsi.
 
Kama huna uelewa ni wewe, vijijini kuna wasomi na kuna watu wengi tu wanamuelewa watanzania sio wajinga hivyo kushindwa kuelewa speech
 
Pitching, pitching, pitching!
Wewe mwenyewe hata hiyo pitching huwezi kuielezea vizuri.
Hotuba ya mama SSH mbona iko poa tu! Labda utakuwa na matatizo yako binafsi.
Nawe acha kuisikikiza akili Yako isiyo na akili! Rais Kasema kuwa akiba ya fedha za kigeni tunazo dollar za marekani bilioni elfu 6,523 ambazo ni zaidi ya deni tunalodaiwa na Bado zinabaki!
Mwananchi wa chini kabisa unadhani atamwelewa rais huku bei za huduma muhimu zikiwa juu naye kayahifadhi matrilioni ya shilingi BoT?
Hii ndio pitching inayozungumziwa hapa kwamba ikampitch mwananchi wa kawaida! Elewa.
 
Wabongo tupunguze ujuaji
 
Sijaona tatizo,wabongo tupunguze ujuaji
 
Pitching ni nini?
Simply put, a media pitch is an attempt to get a journalist/editor or media outlet interested in your news so that they decide to cover it.
 
Mheshimiwa Rais, Mama yetu SSH, Watanzania tulio wengi tumefarijika na hotuba yako ya salamu za mwaka mpya.
Nina imani kubwa Watanzania wengi wanakuombea kheri ya Afya ili uendelee kutuongoza vizuri.
Mama kipenzi cha Watanzania, kama itakupendeza, naamini una mkono mrefu, mfuatilie Kanali Sawala, Mkuu wa Wilaya ya Newala aje aongezee nguvu kwenye jopo lako la watu wanaoandaa hotuba zako, huyu mtu ni mzuri, anajua nini kiandikwe.
Halmashauri kuna vijana wazuri wanaandika hotuba hawajaonekana tu.
Nikutakie mwaka wenye kheri Mama yetu, Kwa muda mfupi umeonyesha matumaini makubwa kwa Nchi yetu, haijawahi tokea kwa muda mfupi wa miezi miwili vijengwe vyumba vya madarasa zaidi ya15,000, vituo vya Afya zaidi ya mia mbili, hospital, Shule mpya zaidi 26, mabweni, barabara kila jimbo.
Watanzania tuko pamoja nawe.
 
Hili la kupeleka mabilioni zanzibar inaonyesha namna gani huyu mama alivyodhamiria kutumia hiyo nafasi kuinufaisha zanzibar.......ni bora tupewe takwimu za namna zanzibar itakavyoshiriki kulipa mgao wake wa mkopo.
 
Mbona mwandiko kama wa Kanali Sawala
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…