Viongozi wa umma wengi hawajui sheria (Law) ndio maana hata utendaji wao wa kazi kila muda una ukakasi. Wanafanya mambo kama wendawazimu.
Sheria ni mkusanyiko wa vitu vitatu,
1) Maadili (Moral & Ethics).
2) Desturi (Custom).
3) Uhalali (Legality).
Kuna wakati sio lazima kufuata sheria moja kwa moja katika utendaji wa kazi, sometimes inahitajika busara (Common Sense/Reasoning), desturi au maadili kwenye utendaji na maamuzi.
Mfano,
Mahakama mara nyingi hutumia theory ya "Reasoning/Common Sense To A Lay Man" (Ratio Decidendi) kwenye kutoa maamuzi.
Unakuta mtu ameua na anashtakiwa kwa kosa la kuua, sheria inakataza vikali kuua na imeweka hukumu kali sana kwa mtu atakaeua, mwisho wa kesi mahakama inamwachia huru mtuhumiwa huyo (Sio bila sababu tu kwamba hana hatia ya kuua au hajaua, ni kweli ameua ila anaachiwa huru kwa kutumia reasoning ya kwanini amefanya hilo kosa - Maybe ameua kwa self defence (Kujihami), maslaughter (Kuua bila kukusudia kama vile ajali), provocation (Uchochezi, mtu alikua provoked kuvuka mipaka), insanity (Kupatwa na wazimu).
Mahakama ingekua inasimamia sheria kama sheria inavyotamka, bila kutumia busara na hekima kwenye kutoa maamuzi, hata watoto wadogo, vichaa na wendawazimu wangefungwa magerezani (Hata wanaofanya makosa bila kukusudia wangejaa mahabusu).
HICHI NDIO MAMA SAMIA ALICHOMAANISHA - Sheria ipo flexible, viongozi wa umma nao wawe flexible kwenye kufanya maamuzi, waangalie madhara ya maamuzi yao wanaotoa.
PRAYERS ZETU:
Mama Samia na yeye kwa upande wake afanya hili jambo kwa mifano hai, afute sheria zote alizoweka Magufuli ambazo hazipo flexible ambazo ni za "KUKOMOA, KUNYANYASA NA KUKANDAMIZA (Raia, Waandishi Wa Habari, Vyombo Vya Habari, NGO, Wafanyabiashara, Kuzuia Takwimu Kuchambuliwa n.k)"