GUSSIE
JF-Expert Member
- Dec 2, 2014
- 3,880
- 11,134
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam bwana Albert chalamila juzi alikiri mbele ya Rais Samia siku ya upokeaji wa taarifa ya haki jinai nchini kuwa sasa ameacha ujinga na kuruka ruka kuwabughuzi wananchi bali atazingatia sheria, taratibu na kanuni za nchi.
Albert Chalamila mbele ya Rais Samia aliwasimamisha mkuu wa wilaya ya ubungo na kinondoni kuwa hawafuati sheria kwa kuwabughuzi raia, alikiri amewaambia wakuu wake wa wilaya mbele ya Rais Samia wajirekebishe.
Dunia ilishabadilika na huwezi kuyazuia mabadiliko, Misimamo ya kidini na ya kiimani haiwezi kuwabadilisha raia bali kufuata haki, kanuni na taratibu ndizo zitakazobadilisha raia. Hakuna zuio la watu kwenda guest, hakuna zuio la watu kwenda bar na wala hakuna zuio la watu kuvaa nguo fupi kwenye miongozo yetu tukiwa sehemu za starehe au Faragha
Mkuu wa mkoa aliyelawiti raia alianza kama huyu kwa kujifanya kufoka foka mara kukamata raia kumbe ana ajenda zake za siri, Pengine mkuu wa wilaya ni mzoefu wa hao Dada poa lakini cheo kinambana sasa anakuja kwa mbinu mpya
Mkuu wa wilaya ya ubungo Dar es Salaam anaongozwa na misimamo ya kiimani na kidini na hili ndilo kosa kubwa la uongozi, Dini na imani yako ni huko makanisani, Misikitini na kwenye Temples. Nchi inaongozwa kwa sheria, taratibu na kanuni
Waziri Nape Nnayu siku ya kikao cha Rais Samia na wanahabari alijaribu kuchombeza kuwa wao jioni watakuwa na sherehe moja kabambe na vibe la kutosha anamuomba mkuu wa mkoa Albert Chalamila na watu wake yaani polisi wasije ingilia starehe zao watakazo zifanya usiku na wanahabari.
Jambo la kushanhaza hao waliokamatwa na mkuu wa wilaya ubungo anaowaita wanajiuza amezuia wasipewe dhamana na wala wasionane na ndugu pamoja na familia zao.
Je, Mkuu wa wilaya ya ubungo hiyo nguvu ya kuwa juu ya sheria na kupingana na ripoti iliyowasilishwa kwa Rais anaitoa wapi? Rais Samia alisisitiza kuwa ndani ya ripoti inaonyesha baadhi ya wakuu wa wilaya hawafuati sheria.
Mkuu wa wilaya ya ubungo chini ya Albert Chalamilan amejigeuza hakimu,Polisi na Afisa upelelezi katika sakata lake la kuvamia nyumba za kulala wageni pamoja na sehemu za kuuzia vileo maarufu kama Bar.
Baadhi ya watu aliowakamata walikuwa kwenye starehe zao wanakunywa pombe na hili sio kosa kisheria ,Unavamia Bar watu wanakimbia hovyo halafu ukiwakamata unasema wanajiuza.
Baadhi ya watu walikuwa wamevaa vimini na hata maofisini kwa sasa ndio mavazi ya dada zetu maofisini na hata wake zetu wanavaa nguo fupi waweze kuendesha magari kwa uhuru ,Je utaendesha gari na dela,Na hakuna kosa la mtu kuvaa nguo fupi hapa Tanzania.
Ni jambo la kushangaza na kusikitisha sana mkuu wa wilaya ya ubungo aliyesimamishwa mbele ya Rais Samia na mkuu wake wa mkoa bado amekuwa kichwa ngumu anazuia dhamana kwa watu ambao yeye sio mpelelezi bali amehisi wanajiuza kwa kuvaa nguo fupi na wengine wakiwa Bar.
Rais Samia fukuza kazi mkuu huyu wa wilaya ubungo kabla hajaharibu kama yule mkuu wa mkoa aliyelawiti raia.