Rais Samia Hakuhitaji Kiapo cha Urais

Sababu ya kiapo kwa Rais, au Jaji, au Waziri, au RC, au DC, au mbunge, nk. si kutangaza lini madaraka ya mhusika yanaanza; bali ni kuwathibitishia wananchi mbele ya Mungu kwamba mhusika anaahidi kutimiza majukumu anayokabidhiwa kama ipasavyo. Tarehe ya kuanza majukumu hutangazwa pekee na huenda ikawa tofauti na siku ya kula kiapo. Ndiyo maana hutangazwa kwamba uteuzi huo utaanza tarehe fulani. Kwa hiyo madhumuni hasa ya kula kiapo ni hilo la kuahidi kutimiza kazi kiadilifu. Siyo kuashiria madaraka yanaanza lini.
 
Mto
Mtoa mada ametoa hoja zake kwa uadilifu na kukariri mambo kadhaa kutia nguvu hoja anayojenga. Hii ni mada nzuri na hivyo ndivyo inavyotakiwa katika uwanja hu wa JF wa Great Thinkers. Badala yake, nimeona baadhi ya wachangiaji wanaingiza mambo ambayo hayahusiani kabisa na mada. Kwa mfano, mmoja amesema 'tunahitaji katiba mpya'. Sasa hili linahusika vipi na mada husika? Mwingine akasema kama CCM ingekuwa inafuata Katiba, ingekuwa imekwishatoweka zamani. Tafsiri ya kauli hiyo ni kwamba Katiba ni nzuri. Kasoro ni kwamba haifuatwi. Vivyo hivyo michango mingi imejikita katika mambo ya Katiba, kitu ambacho mtoa mada hakukidhamiria katika uzi huu. Michango kama hiyo inashusha hadhi ya jukwaa hili la Great Thinkers. Kama una tatizo na Katiba, anzisha uzi wako juu ya somo hilo. Siyo kuchafua uzi wa mwenzako.
 
Asante kaka,

Hata mim sitaki kupata sifa ya mtoa mada. Nimeeleza kwamba hii makala niliiona niliposoma gazeti la RAIA MWEMA.

Makala iliandikwa na Joseph Magata.


 
Asante kaka,

Hata mim sitaki kupata sifa ya mtoa mada. Nimeeleza kwamba hii makala niliiona niliposoma gazeti la RAIA MWEMA.

Makala iliandikwa na Joseph Magata.
Asante kwa ufafanuzi. Kwa ufupi ni kwamba makala ya Magata ilikuwa ya kisomi hasa. Hata kama msomaji hukubaliani na hoja zilizotolewa, ruksa kwako kuzikosoa hoja hizo. Siyo kuanza kulalamikia mambo ambayo hayakudhamiriwa kwenye mada.
 
Kwenye list umemsahau Pole Pole, Gwajima na yule DPP wa zamani!
Hakika CDF na JK walicheza kuliokoa Taifa.
Nakumbuka pilika pilika kabla ya ule usiku wa tangazo la msiba na yaliyojiri baada ya pale.. Yaani unaona kabisa serikali ilikuwa imetekwa nyara!
 
Ni lini Tanzania imeanza kutumia katiba? Tungekuwa tunatumia katiba japo robo tu hiyo ccm ingekuwa imeshafutwa siku nyingi ni genge la kigaidi tu sawa na Al qaeda tu.

Na huu ndio tunaita uozo wa mawazo

Mnakaa kufikiri hiyo katiba mpya ndio suluhu na njia pekee ya kuwatoa CCM madarakani na kuwaweka wapuuzi wasiojielewa madarakani na sio kufikiri namna gani Katiba mpya inaweza kuleta chachu na tija ktk maendeleo ya nchi
 
Kabisa Mkuu, bila CDF Mabeyo tulikuwa tumekwisha poteana
 
Kila kitu kuhusu urais wa Samia ulivyokuja kimeelezwa huku kwenye huu uzi.

 
Hawataelewa
 
Nadhani tulikuwa chini ya Kaimu Rais, immediately baada ya JPM kuwa ametwaliwa na Bwana.
Je, Kaimu Rais anahitaji kuapishwa?
By the way, bila kuapishwa Kaimu Rais hana mamlaka ya kufanya baadhi ya mambo fulani fulani mithili kusaini au kufuta hati za hukumu za vifo; kwa watu waliohukumiwa kunyongwa.

Umeandika hapa mengi na ninadhani wewe ni mwanasheria. Unadhani ilikuwa ni busara kwa Kaimu Rais kuapishwa immediately, after an hour or so, baada ya JPM kutwaliwa na Bwana? Huoni kwamba hapa Katiba ingetumika kuu-override ubinadamu, na hivyo sheria kuwa ya muhimu zaidi kuliko ubinadamu? Au hoja yako hapa ni kwa sababu Wamarekani wana mechanism yenye mchakato ambao si sawa na wa kwetu?
Issue unayojaribu kutuleleza sisi hapa ni ipi hasa? Ni kwamba tulifanya makosa kwa sababu tu tulifanya tofauti na wanavyofanya Marekani, au?
 
Nilikwambia, hawataelewa na wengine hawatasoma kabisa kama huyu anaishia kudhani.

 
- - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - -
Makundi yaliibuka ya kuipinga na kuiunga mkono TLS, lakini yote hayakuonyesha historia ya viapo. Makala hii inaonyesha historia hiyo ilivyo msingi usioepukika wa jambo hili.
?????????????!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Kwa hiyo Katiba inasema pia kuwa TLS ndiyo wana mamlaka ya kushauri nani anatakiwa kuapishwa, au waliamua kushauri tu kwenye swala hili specific kwa sababu wao ni mahiri wa mambo ya sheria?
 
Ndiyo maana Samia anasema Katiba mpya si hitaji la wengi maana hamuijui hata ya sasa, kama wewe.

?????????????!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Kwa hiyo Katiba inasema pia kuwa TLS ndiyo wana mamlaka ya kushauri nani anatakiwa kuapishwa, au waliamua kushauri tu kwenye swala hili specific kwa sababu wao ni mahiri wa mambo ya sheria?
 
Ndiyo maana Samia anasema Katiba mpya si hitaji la wengi maana hamuijui hata ya sasa, kama wewe.
Hujajibu swali. Ungejibu swali kwanza halafu ndiyo unituhumu kuwa sijui. Nauliza tena; je; Katiba inasema pia kuwa TLS ndiyo wana mamlaka ya kushauri nani anatakiwa kuapishwa, au waliamua kushauri tu kwenye swala hili specific kwa sababu wao ni mahiri wa mambo ya sheria?
 
Muulize mwandish wa makala.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…