Rais Samia hakupita jeshini, Rais Mwinyi hakupita Jeshini. Wabunge wengi pia hawakupita jeshini, nchi ina tatizo

robinson crusoe

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2020
Posts
842
Reaction score
1,425
Sehemu kubwa ya hawa wote niliowataja, ndo wanachochea matumizi ya vyombo ya ulinzi ktk amani ya nchi. Bahati mbaya baadhi yao hawakwenda jeshini kwa kukwepa sheria iliyokuwepo. Yawezekana kabisa hawafahamu matokeo ya maneno yao juu ya vyombo vya ulinzi wa nchi.

Huko bungeni pia kuna wabunge wasiojitambua. Wakizungumza wanatoa amri za ukali utadhani ni makamanda kuliko hata jeshi. Wanalisemea jeshi uwezo wake wakati hata hawakupitia jeshini.

Je, tufanyeje ili viongozi hawa waweze kuelewa madhara ya kutoa amri kwa vyombo vya ulinzi?
 
Huwa wanashabikia kwamba JKT inaongeza maadili. Ina maana tunaongozwa na watu wasio na nyongeza ya maadili. Siyo ajabu pembeni wanateta sana juu ya 'ujinga' wa waliopita jeshini.
 
Iwapo tu walitaka kuliingilia jeshi kwenye Ajira zake za kuandikisha itakuwaje mengine ya kimaadili ya jeshi. waziri wa ulinzi aliwaonya.
 
Kwenye katiba mpya, hii ya kupita JKT kwa mgombea urais ni vyema ikawa moja ya masharti ya lazima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…