SI KWELI Rais Samia Hakuwadhihaki Wanaume Wa Kenya Kufuatia Uchumba Wa Charlene Ruto

SI KWELI Rais Samia Hakuwadhihaki Wanaume Wa Kenya Kufuatia Uchumba Wa Charlene Ruto

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Machapisho yanayosambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii yanadai kuwa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan aliwadhihaki wanaume wa Kenya kufuatia uchumba wa Charlene Ruto na mfanyabiashara Mtanzania Isaya Yunge.

1786361629276.png
 
Tunachokijua
Hakuna taarifa, kauli rasmi wala taarifa kwa vyombo vya habari kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan au Ikulu ya Tanzania inayothibitisha madai hayo.

Kauli zinazodaiwa kutoka kwa Rais Samia zinazoenezwa mtandaoni zinaonekana kuwa zimetoka kwenye kurasa za kejeli (satirical pages) na vyanzo bandia vya habari, vilivyolenga kuchochea mijadala na kupata usikivu.

Kwa sasa, hakuna ushahidi wa kuaminika unaoonyesha kuwa Rais Samia aliwahi kutoa kauli hizo kuhusu wanaume wa Kenya au uhusiano wa Charlene Ruto na Isaya Yunge.
The image circulating on social media features a fake quote maliciously attributed to Tanzanian President Samia Suluhu Hassan.
1786271040267.jpg
 
Back
Top Bottom