Notorious thug
JF-Expert Member
- Dec 29, 2021
- 2,817
- 10,667
Poleni na majukumu ya kila siku wana jukwaa.
Wiki mbili zilizopita nilikua Kanda ya Kaskazini mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Tanga nilipata bahati ya kutembelea Magereza ya Karanga(Kilimanjaro-Moshi) Kisongo(Arusha) na Maweni(Tanga) niliona vijana wadogo umri miaka 19-23 wakiwa gereza washahukumiwa katika kudodosa dodosa kati yangu na baadhi ya Maaskari Jela wengi wa wale Vijana wanatumikia vifungo virefu miaka 30 hadi maisha kwa makosa ya dawa za kulevya(Bangi na Mirungi) ambapo kwa mujibu wa sheria ya kupambana na kudhibiti madawa ya kulevya Tanzania(Marekebisho-2017) Wengi wamejikuta wakitiwa hatiani na kuhukumiwa vifungo virefu.
Ombi langu kwako Raisi Samia Hassan Suluhu naomba uwaangalie kwa jicho la huruma wale wote waliokwisha kutumikia kuanzia miaka 5-10 waweze kuandaliwa utaratibu maalumu wa kuachiliwa huku vienendo yao ikifuatiliwa wengi wanajutia makosa waliyoyafanya na wapo tayari kubadilika. Kutokana na kesi hizi wengi wameuza Viwanja na Nyumba kuhonga kumaliza kesi ila imeshindikana Familia,Wazazi na ndugu wamekua Maskini kutokana na kesi hizi.
Kwako Raisi Samia Suluhu naomba usikilize kilio hichi cha Vijana wako walioko Magerezani wanakulilia Mama wanaomba waione tena nuru Magereza imewafundisha wanajutia makosa yao pia Mama angalia na Wazee waliopo Magerezani na Walemavu waliopo magerezani wape msamaha waje kuliona jua uraia wakielekea mwishoni mwa maisha yao.