Rais Samia: Hatua yoyote tunayoichukua kama Serikali ni kwa faida ya wananchi

Body language na uhalisia wake ni vitu viwili tofauti.
Nyie mmeamua kumchukia tu Samia kwa vile anatoka upande wa 2 wa Muungano na kwa jinsia yake. Lakini ninakuhakikishia kuwa kazi aliyopiga kiuchumi, miundombinu, elimu na afya ni ya kutukuka.

Pengine hata hao ambao mlitaka wachukue nchi baada ya Magufuli wasingetufikisha hapa.
 
Analoweza ni kukopa na kutokulipa.
Deni la mama limefika Tirion 107.

Magufuli wakati anaingia madarakani deni lilikuwa Tirion 43 hadi anafariki deni lilikuwa Tirion 65.
Unaona mikopo tu kwani kazi alizofanya huzioni? Huyo Magufuli alianzisha miradi mkakati kama 4 kwa wakati mmoja na mpaka anakufa hakuna mradi ulikuwa 50%.

Je mlitaka aiache miradi hiyo kwa vile akikopa mtamsema?
 
Unaona mikopo tu kwani kazi alizofanya huzioni? Huyo Magufuli alianzisha miradi mkakati kama 4 kwa wakati mmoja na mpaka anakufa hakuna mradi ulikuwa 50%.

Je mlitaka aiache miradi hiyo kwa vile akikopa mtamsema?
Kwani alilazimishwa kufanya hiyo.miradi?
Kulikuwa na ulazima wa kukopa ili kufanya hiyo miradi?
 
Kwani alilazimishwa kufanya hiyo.miradi?
Kulikuwa na ulazima wa kukopa ili kufanya hiyo miradi?
Mkuu hivi unazo akili hata kidogo au nabishana na ZWAZWA? Yaani unauliza kuhusu kuacha kumalizia Bwawa la Nyerere au SGR??
 
Mkuu hivi unazo akili hata kidogo au nabishana na ZWAZWA? Yaani unauliza kuhusu kuacha kumalizia Bwawa la Nyerere au SGR??
Nina akili kulipo wewe embu nitajie faida ya hilo bwana la umeme hadi sasa hivi?
Umeme haukatiki? Bei ya umeme imeshuka ?
Hiyo sgr nayo ni hasara tusubir ripoti ya cag mwaka ujao wa utasikia.
Acha kusifia upumbavu kichawa .
Nyie machawa ndio hamna akili mnatetea hata upumbavu
 
Wewe ni mpumbavu ila hujijui. Kubishana na wewe ni kumpigia mbuzi guitar
 
Asilimia kubwa hatua zinazochukuliwa ni hasara kwa wananchi. Tena kubwa sana!
 
Hatua ya kuuza bandari na kuamisha wamasai? Au kua n kuteka?
Kazi ni kipimo cha utu
 
Aanze kwa kuwaeleza wananchi Gesi ya Ntorya, kule Mtwara, waliyopewa waOman inawanufaisha vipi wananchi.

Wamasai waliohamishwa Ngorongoro, wananufaika vipi na eneo lao kupewa wageni na wao kuhamishwa kwenye makazi yao.

Awaeleze wananchi wa Tanzania, kwa nini mapori yao wanagawiwa watu toka nje, kwa jina la uwekezaji wa "Carbon Credits"; uwekezaji huo wa kutunza mapori waTanzania hawawezi kufunzwa na kunufaika nao?

Awaeleze wananchi inakuwaje waTanzania hawawezi kamwe kuendesha bandari zao, ilazimu kuleta wageni kufanya kazi hizo

Na hasa hasa, anatakiwa awaeleze wananchi; hilo zao la pamba halikuanza leo hapo Simiyu. Miaka yote aliyokuwa serikalini hakujuwa uwepo wa zao hilo? Amesahau kuwa hizi kampeni za kukuza zao hilo zimekuwepo hapa tokea miaka mingi; sasa kwa nini aje tena kwa hadaa za kuwarubuni wananchi?
 
Umemuua mwananchi sasa ni kwa faida ya mwananchi gani kama umeshamuua tayari mwananchi,boya sana huyu mwanamke.
 
Stay tuned and reserve your comments until when she will address issues related to peace, abductions and tranquility
I'll be the first to applaud her if she does that! However, I highly doubt she has the temerity of doing that.
On agriculture, there's nothing new; its empty/hollow talk as expected. Cotton has been here for quite sometime, and it's only a few years back there were feeble efforts towards resuscitating the crop to no avail. The little that farmers were able to produce had to be shipped out to Kenya to feed their textile industries! And you call tahat leadership?
 
Hatua pekee itakayokuwa na faida kubwa na kufanya apendwe milele ni kutangaza kutogombea tena.
Angekuwa na fahamu hiyo asingehangaika kama anavyofanya sasa.

Ni wazi kabisa sasa kuwa huyu yupo tayari kwa lolote lile litakalombakisha madarakani.

Huyu hana hata chembe ya kuachia ngazi kwa salama ya taifa hili.
 
Mazao ya kilimo yanauchangia mkubwa pato la taifa Tanzania (Gross Domestic Product - GDP), hasa kwa kuwa sekta ya kilimo inachangia takriban 26-30% ya GDP na kutoa ajira kwa zaidi ya 70% ya wakulima. Hapa kuna mchoro (graph) wa mchanganuo wa mazao muhimu ya kilimo yanayochangia uchumi wa Tanzania
 
Kipya hapa ni kipi hasa! Sioni sababu ya kunionyesha hizi tarakimu hapa!
Isipokuwa kubaki tu tunashangaa nchi kama hii yenye baraka tele kuwa takwimu za aina hiyo.
BTW: Takwimu hizi zimekuwepo miaka na miaka; hazibadiliki kwa kiasi kikubwa!

We certainly can do much, much better than this.
Kama kuna eneo ambalo waTanzania wengi wangeweza kubadili hali zao za maisha kwa haraka zaidi, ni hili la kilimo.
Sixty years, bado tuna kilimo chenye kutoa takwimu za aina hii?

Unajuwa mkuu 'Stuxnet', unaweza kuniuliza habari za "Kilimo ndio Utii wa Mgongo", na 'iterations' zake mbalimbali na ukapata jibu.
Sasa sijui ulikuwa na lengo gani la kuweka hizi tarakimu hapa, maana sioni zikijibu hoja yoyote!
 
Kuua si kwa manufaa yetu sisi wenye dini ila ni kwa manufaa ya serikali isiyo na dini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…