My Son drink water
JF-Expert Member
- Nov 30, 2016
- 4,932
- 13,306
Zoezi la kuiua CHADEMA alilianza Hayati Magufuli na kaondoka Duniani hajafanikiwa kuiua CHADEMA. Kwa maneno mengine rahisi, aliyetaka CHADEMA ife kafa yeye na kuiacha CHADEMA ikiwa hai.
Mbowe alikuwa hana tuhuma zozote za Ugaidi hapo kabla, lakini alipoanza vuguvugu la kudai Katiba Mpya mkamkamata na kumbambikia kesi ya kigaidi.
Police wanatoa hoja za kitoto za kuwafanya watu wote hawana akili. Eti walikuwa wakimchunguza na sasa wamepata ushahidi na kumkamata.
Swali kwa Police: Utamchunguzaje suspect huku akiwa huru? What if akitoroka?
Rais Samia, tunakuheshimu sana kama Rais wetu, lakini hatukuogopi. Tunayemwogopa ni mmoja tu, naye ni MUNGU.
Hakuna wa kututisha kuhusu kudai Katiba Mpya, tutaendelea kuidai kwa njia nyingi tofauti hadi tutaipata, na njia kubwa kuliko zote tumeanza kukushtakia kwa MUNGU. Kama utaweza kushindana na MUNGU basi CHADEMA itakufa, lakini kwa sababu Mungu huwa ni wa haki,atasimama kwenye haki.
Rais Samia, hautafanikiwa kwenye njama zako za kuiua CHADEMA, Mbowe siyo CHADEMA. Nyie mfanyeni vyovote vile mnavyojua, lakini mtakapoanza kulipa ghadhabu ya MUNGU msikimbiane humo.
Huwa mnajiona mna haki sana ya kufanya lolote, wakati ni ukuta, iko siku hamtavuka.