OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Hii nchi na viongozi wake wanasikitisha sana. Moja kati ya 4R alizokuja nazo Rais Samia ni Mabadiliko (Reforms). Samia alisisitiza mabadiliko katika sekta mbalimbali ili kuboresha maisha ya wananchi.
Katika maendeleo na maisha ya wananchi huwezi kuweka pembeni Siasa. Siasa ndio inaamua hatma ya maendeleo na maisha ya wananchi. Katika siasa huwezi kuweka pembeni Uchaguzi. Uchaguzi ndio mkakati mkubwa wa wananchi kuchagua watu wa kuwaletea maendeleo. Kwa lugha rahisi ni sekta muhimu.
Sekta ya siasa na uchaguzi limekuwa eneo linalopigiwa sana kelele sio tu na upinzani bali hata CCM kwenyewe wameonyesha kuna mapungufu. Wote tumesema uchaguzi wa 2020 ulikuwa wa hovyo kabisa na ulizaa chuki kubwa na kusababisha majeraha. Maana yake ilihitajika Reform ikiwa integrated na R nyingine ya Maridhiano.
Ajabu ni kwamba yule mtu anayemkumbusha Rais Samia juu ya Reform anaonekana kituko. GT tunajua Tundu Lissu hana jipya kuhusu Reform kwa sababu ameiba kwenye 4R za Mama. Researchers tunasema Lissu kafanya Plagiarism kwa Mama (maana hakuwahi ku-acknowledge).
Ajabu ni kwamba Mama mwenyewe anashangaa huyu Tundu Lissu vipi anayatoa wapi haya mambo ya ajabu? Waliofuatilia bunge maalumu la katiba wanakumbuka jinsi Mwakyembe alivyogeuka kituko. Kwenye tafiti yake aliandika mambo mazuri kuhusu serikali tatu. Lakini ajabu lilipokuja suala la utekelezaji kikatiba akaipinga serikali tatu. Hiki ndicho anachofanya Rais Samia, kwenye makaratasi ameandika 4Rs ikiwemo Maridhiano na Mabadiliko lakini anapotakiwa kutekeleza anashangaa hivyo ni vitu gani!
My Take
Nimekuja hapa kuwakumbusha tu. Sina ushauri wowote kwa sababu naelewa The governance of this country is damaged beyond repair
Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025