Shujaa Mwendazake
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 4,016
- 6,759
Ni wiki sasa tukianzia kule Zanzibar tumeona kamati ya Uongozi ya CCM ikifanya mikutano ya kisiasa , lakini pia nimeona trend ya Chadema wakiendelea na oparesheni haki kwenye mikoa mbalimbali hapa nchini japo nadhani wao wanafanyia ndani (sina uhakika).
Lakini Mh Rais alikuwa ametoa kauli kuwa mikutano ya kisiasa isubiri kwanza au wahusika (Wabunge, Madiwani, wenyeviti wa mitaa) wafanye kwenye maeneo yao tu. Hili lilileta taharuki kubwa sana mitandanoni lakini kama tujuavyo kauli ya Mh Rais ni kubwa kama tulijione awamu iliyopita vyombo vya dola vilizuia mikutano mingi kwa agizo la Shujaa na kwa taarifa za Kiintelijensia.
Sasa tunachojiuliza, hii kamati ya uongozi ya CCM ikiongozwa na Katibu mkuu, Bw Chongolo na Shaka Hamidu ni kuwa hawakumuelewa Rais wetu mpendwa, wau walimuelewa bali wamekaidi au wanamuona kama Mama kuwa hawezi kuwachukulia hatua?. Lakini pia vipi vyombo vya dola wakiachia agizo hili la Rais kuzuia Mikutano ya kisiasa Mfano Kamati za uongozi kuzunguka nchini kufanya siasa.
Nitoe Rai kwa Mh Rais kukemea hili, lakini pia vyombo vya dola kuwachukulia hatua ama kutoa Muongozo wa aina gani ya mikutano inayoruhusiwa na isiyoruhusiwa na kwa vigezo vip.
Lakini mwisho na ndiyo hofu yangu ilipo ni kuwa Labda Mheshimiwa Rais na mama yetu mpendwa Samia Suluh Hassan hakueleweka ama alitoa kauli yenye utata na iliyokuwa haijakamilika ujumbe wake. Tunategemea Msajili wa vyama vya Siasa atoe huu Muongozo ama Chama cha Mapinduzi kichukuliwe hatua kwa kukiuka agizo la Rais.