Rais Samia huwa anatumia vigezo gani katika teuzi zake?

Rais Samia huwa anatumia vigezo gani katika teuzi zake?

mshale21

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2021
Posts
2,126
Reaction score
5,068
Wakuu, Rais wetu mara kadhaa amekuwa akiteuwa na kutengua teuzi zake, pia amekuwa akibadili majukumu ya viongozi mara kwa mara, mara hii hadi kaamua kumrejesha mtu aliwahi kumtumbua katika position ile ile!

Sasa maswali ni je, huwa anazingatia Nini hasa katika teuzi za viongozi mbalimbali?

Nini kinapelekea afanye mabadiliko ya mara kwa mara kiasi hicho?

Wajuvi wa mambo karibuni tutoane tongotongo.
 
Katiba iliyopo inampa mamlaka ya kutumia utashi wake kufanya uteuzi, na sio yeye tu ni Rais yeyote awaye, usifikirie sana, utajipasua kichwa bure.
 
Hata Magufuri aliwahi mtumbua Mwigulu Nchemba na Simbachawene lakini baadaye akawarudisha tena kwenye madaraka.
 
Katiba iliyopo inampa mamlaka ya kutumia utashi wake kufanya uteuzi, na sio yeye tu ni Rais yeyote awaye, usifikirie sana, utajipasua kichwa bure.
Na hili ndio jibu la swali kwa mleta mada. Hadi hapo hizi nafasi zitakapopatikana kwa vigezo, bado taifa lina safari ndefu sana.
 
Teuzi za kisiasa hazina vigezo maalumu zaidi ya kujua kusoma na kuandika
 
Teuzi za kisiasa hazina vigezo maalumu zaidi ya kujua kusoma na kuandika
 
Hata Magufuri aliwahi mtumbua Mwigulu Nchemba na Simbachawene lakini baadaye akawarudisha tena kwenye madaraka.
Tuna safari ndefu kuelekea ukombozi kutoka kwenye mikono ya wanasiasa. Ndo umejibu swali/maswali ya mleta mada?
 
Back
Top Bottom