Rais Samia ikikupendeza mfute kazi RC wa Mara, Ally Hapi kwa Kushindwa Kuisafirisha Biashara United FC kwenda Libya

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Haiingii Akilini kwa Uyanga wake Pesa za kuwapa Timu Pinzani ( hasa hiyo ya Biashara United FC ) ya Mkoani Mara na hata ile ya Lipuli FC ( alipokuwa Iringa ) kila zikikutana kucheza na Timu anayoichukia ya Simba SC huwa anakuwa nazo lakini Pesa za Kuisaidia Biashara United FC kusafiri kwenda nchini Libya kucheza Mechi yake ya Kimataifa ya Kombe la Shirikisho hana.

Kitendo cha Klabu ya Biashara United kushindwa kusafiri kwenda Libya si tu Kimeiabisha Tanzania, Wewe Mwenyewe Rais Samia ila Kimeiabisha pia Serikali nzima ya Mkoa wa Mara ( Musoma ) iliyo chini ya Mkuu wa Mkoa 'Mnafiki' Ali Hapi kwa Kushindwa Kwake kuja na 'Mikakati' thabiti ya Kuisaidia hii Timu.

Marehemu Lawrence Gama Mkuu wa Mkoa Mfano bora kwa Wakuu wa Mikoa wapenda Michezo aliweza Kuziimarisha Timu zote zilizokuwa katika Mikoa aliyokuwa akiiongoza huko Ruvuma, Tabora na Morogoro ( kama sijakosea ) na kuja kuwa Tishio katika Ligi Kuu na hata Mashindano ya Kimataifa.

Haiingii Akilini kipindi cha Marehemu Gama hali ya Uchumi ya nchi ilikuwa nj mbaya ila Mzee Gama aliweza kufanya 'Mobilization' ya Watu Maarufu, Wafanyabiashara na Wananchi wa Kawaida kuweza Kuzichangia Timu za Mikoa yao kiasi kwamba Kilio cha Ukata ( Umasikini ) kulikuwa hakisikiki na hata Mikoa hiyo baadae ilikuja kusifika kwa kutoa Vipaji vingi na vikubwa vya Soka.

Leo hii Mkoa wa Mara ( Musoma ) ambao una Rasilimali za Kutosha ( kama Madini) na Kivutio cha Mbuga Kubwa ya Wanyama ya Serengeti huku kukiwa na Wafanyabiashara wakubwa na Matajiri wa Viwanda, Makampuni na Uvuvi lakini Mkuu wa Mkoa wa 'hovyo' Ali Hapi ameshindwa Kutumia vyema Akili zake na kuwa 'Mbunifu' Kuisadia Klabu ya Biashara United FC ya Mkoani Kwake Mara Kusafiri kwenda nchini Libya ila kutafuta Pesa za 'Kuihujumu' Simba SC kila ikicheza na Timu za Mikoa anayokuwa huwa anazo, hakosi na anajua anakoweza kuzipara tena kwa haraka kabisa.

Mama ( Rais ) mfukuze tu huyu Mnafiki.
 
Asimsahau na Dc wake aliyebomoa ofisi za Chadema huko Bunda.
Kwahiyo hili 'Dukuduku' la huyo DC wake ulikuwa unalo Siku nyingi na ulikuwa unasubiria tu upate 'Lifti' ya Kuliwasilisha ( Kulifikisha ) kwa kupitia 'Threads' za Watu wengine na Wewe umeshindwa Kumuanzishia Mada ( Uzi ) hapa JamiiForums Mkuu au?
 
Kwahiyo hili 'Dukuduku' la huyo DC wake ulikuwa unalo Siku nyingi na ulikuwa unasubiria tu upate 'Lifti' ya Kuliwasilisha ( Kulifikisha ) kwa kupitia 'Threads' za Watu wengine na Wewe umeshindwa Kumuanzishia Mada ( Uzi ) hapa JamiiForums Mkuu au?
Yaani hapo Ni kwny godown aliona aanze kufanya chochote kile video zake mjini anadunda to mpk mida flani hulikosi kwny wilaya ya kinondoni na pia barakoa Ni sawa Ni competitors.
 
Hivi inasound vipi huko nje wananchi wa nchi hiyo wakisikia timu fulani ya Tanzania imeshindwa kusafiri kwa sababu za kifedha? Kuna wakati hata timu ya taifa ilikuwa inakosa pesa za kusafiria. Haya mambo nilidhani yalishaisha.

Ila Tanzania sekta nyingi hazijabadilika kama tunavyodhani.
 
kwa hili sikuungi mkono, huu upumbavu wa kutoa pesa ulianzishwa na akina makonda na shigela dhidi ya team zilizocheza na yanga bt kwa wakati huo sisi wanasimba tuliona sawa iweje leo?
 
kwa hili sikuungi mkono, huu upumbavu wa kutoa pesa ulianzishwa na akina makonda na shigela dhidi ya team zilizocheza na yanga bt kwa wakati huo sisi wanasimba tuliona sawa iweje leo?
Hatuna mwana Simba SC Mnafiki na Mpumbavu kama Wewe tafadhali. Acha Kujipendekeza kuwa Simba SC Fan sawa?
 
Umetumia kigezo cha kushindwa kuipeleka biashara United Libya kama Hana sifa za kuwa mkuu wa mkoa wa Mara sio!? Mbona Kama ni hoja dhaifu sanaa, kwani hata akifanikiwa kuipeleka iyo timu Libya italeta tija gani kwa watanzania maskini ambao wengine hawana hata uhakika wa kula Milo miwili kwa siku!!!!
 
Wewe unahoja dhaifu sana bila shaka ni miongoni mwa wenye vyeti feki waliotumbuliwa na mwenda zake.

Wakati mwingine uwe unaficha udhaifu wako , unatia kinyaa .
 
Hii hoja ya kitoto kama sio kijinga

Inatajwa kugharamia timu kwenda Libya unaweza fika million 140-200 sasa hizi anatoa wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…