Rais Samia ingilia kati, TRA watatukwamisha

Niliwahi kusema bila kufukuza Kazi hao mameneja wa Mikoa na kuwapa targets reasonable hao TRA watakyangusha Sana.

Afu ifike mahala Utumishi wa umma uwe ni Kazi za mkataba ,mbona private sector wanaweza? Hii kuwapa watu ensurance huku hawafanyi Kazi ni upuuzi
 
Rais wangu, ukipata nafasi mwite ofsini Kamishna wa TRA nchini, Bwana Alphayo Kidata. Muulize katika mwezi April/May ambao yeye amekua ofisini amekusanya mapato kiasi gani. Akikupa hesabu linganisha na mwezi wowote katika mwaka wowote unaoutaka wewe. Achana na miaka ya JPM ambayo inasemwa kodi zilikusanywa kwa nguvu. Tumia mwezi wowote katika kipindi cha awamu ya nne kwa makadilio. Ukipata majibu, mpe nafasi ya mwisho Alphayo Kidata, aache kukuchezea!!

Rais wangu, TRA ya Tanzania haikusanyi kodi tena. Wanafika ofsini kwa muda, wanakaa kidogo katika meza zao zilizopangwa shaghalabaghala, wengine wanawasha kompyuta wengine hawawashi. Baada ya muda mfupi, wanakusanyana nusu yao wanaondoka. Wao wanasema wanakwenda kufanya kazi za nje. Ndugu Rais, TRA ya Tanzania inafanya kazi za nje kwa ajili ya kazi za ndani zisizokuwepo.

Rais wangu, wakati wote huu wote waliobaki ofsini, hawana cha kufanya. Waranda-randa ofsini na kupiga miayo na soga. Wengine wanasimulia habari za msiba wa JPM. Hakuna lolote linalofanyika kwa sababu hakuna mtandao. TRA hawakusanyi pesa kwa sababu ya mtandao, nchi haikusanyi mapato kwa sababu ya mtandao. Tatizo la mtandao wa TRA limekua sugu katika nchi yetu, linajirudia leo, kesho na keshokutwa. No one cares!! Mtu mmoja ameniambia kuwa jana (May, 26) TRA nchi nzima haikufanya kazi. Yaani kwamba, kwa siku nzima nchi yote haikukusanya mapato kupitia chombo chake kikuu cha makusanyo. Kama taarifa hii ni ya kweli basi tatizo ni kubwa. Nchi hii siku hizi haikusanyi pesa, halafu inatumia pesa zilizokusanywa na wengine. Wenye hofu wanasema zikiisha zilizokusanywa nchi inaweza kuanguka.

Rais wangu, nenda leo TRA Mwenge, TRA Tegeta na TRA Kimara (zote za Da'slama), kwa kuzitaja chache. Ukikuta zote zinafanya kazi na inaonesha zimefanya kazi yake ipasavyo kwa siku tatu nyuma au na zaidi, niwajibishe mimi kwa namna utakayoona inafaa. Tuna tatizo kubwa, katika nchi kubwa namna hii kushindwa kukudanya mapato kwa sababu ya mtandao ni aibu. Huu utaratibu usipoangaliwa, nchi itatufia mikononi. Nchi isiyokuwa na mapato yake haiwezi kulipa mishahara kwa wakati, haiwezi kununua dawa za hospitali, hakwezi kugharamia elimu bila malipo na haitoweza kukamilisha miradi ya maendeleo ya gharama kubwa. Tukiruhusu nchi ifike hapo, ndio tumekwenda na maji tayari.

Rais wangu, juzi mtandao wa Tanesco ulisumbua kidogo katika kununua LUKU. Licha ya taarifa iliyotolewa mapema na Tanesco ya kuomba radhi lakini nchi nzima ilisimama. Waziri wa Nishati akahamaki, akafukuza watu hovyo, Waziri Mkuu akasimama kutoa maelekezo. Baada ya muda mfupi, umeme ukarudi. Tanesco haikusanyi mapato kama TRA lakini tuliwekeza nguvu kubwa usiku na mchana. Mtandao wa TRA hauna uhakika kwa zaidi ya mwezi, unasumbua kila siku lakini hakuna anayejali, Waziri wa fedha hajulikani alipo wala hajali.

Rais wangu, ni kama wote tumeridhika na hali hii. Pesa hazikusanywi kwa wakati kwa sababu ya mtandao, watu wanakwenda TRA na kurudi kila siku halafu muda wa kulipa ukipita mfanyabiashara anatozwa faini (penalty) kwa kuchelewa kulipa kodi. Hivi ndivyo tunavyohuisha bishara na kuvutia wawekezaji katika nchi yetu. Mtu kwenda TRA kulipa kodi moja kila siku ni kero, tunaharibu ratiba za watu bila sabbau. Wanaomkumbuka Magufuli wanamkumbuka kwa mengi, sisi tuendelee kufanya kazi za nje tukirudi ndani nchi itakua hoi bin taaban. Rais wangu, TRA watakukwamisha ukiweza chukua hatua sasa

MenukaJr,
Da'slama-Tanzania.
We mataga tulia. Mama hataki kodi za dhuluma. Period!

HAKI HUINUA TAIFA
 
Uk
Asante kwa uzalendo ila haya yote Samia anayataka mwenyewe, anatafuta sifa kwa lengo la kuibomoa Tanganyika nao watanganyika wamehadaika. Hakika Samia October nchi inaanguka kiuchumi. Najiandaa kujihami kwa kukopa CRDB ila Lawson am mfumo wa kuingiza makato ya mkopo ni kikwazo mwezi mzima sasa. Tanzania imegeuka Kidampa
Ukiwa unayajua yote hayo unashauri nini?
 
Bandiko zuri lakini umekoaea kitu kimoja! Unataka mama alinganishe na mapato ya kodi kipindi cha awamu ya NNE kama kipimo cha kukusanya kodi? Awamu ya NNE wafanyabiashara walipiga sana! Unakumbuka enzi za Home shopping centre!! Leo iko wapi? Makusanyo yalikuwa hayafiki trilioni!! Tusirudi tena kwenye mabilioni! Kimya kimgi kina mshindo mkuu, kwa ninj TRA wameacha kutangaza makusanyo ya kodi? Bila shaka tunapigwa!
hoja dhaifu hiyo eti wako wapi home shooping center kwani huwajui gsm? ndio tatizo kuchelewa kuja mjini hilo
 
Wewe unamsumbua tu mama; hasa na hiyo ya kumwita "Rais Wako", mwishowe atadhani anakufanyia kazi wewe!

Mama yupo 'bize', anarekebisha mambo atakavyo yeye yawe.

Unajuaje, labda hao jamaa zako wa TRA wameagizwa kufanya hivyo kuwapa marafiki zake wafanya biashara nafasi ya kupumua, halafu wewe unakuja hapa na kulialia!

Hao rafiki zake wafanya biashara hawatamwacha adondoke. Kama kutakuwepo na wa kudondoka, ni makapuku kama wewe msiojitambua.

Sasa najua hutapenda sana bandiko hili, lakini nadhani ndilo linalokufaa mtu kama wewe, kama nimekusoma vizuri na kukuelewa kwenye bandiko lako hilo!
 
Uk
Ukiwa unayajua yote hayo unashauri nini?
Ahimize uwajibikaji kwa walipa kodi hali kadhalika kwa TRA bahati mbaya ameanza kwa kuidhoifisha TRA na kuwapa jeuri wafanyabiashara ama walipa kodi. Umaarufu ataupata kwa matendo sio kwa kauli bomoaji ama kauli sifa. Kodi hailipwi comrade tusisubiri miezi 6 kuporomoka kunakuja. Mungu atusimamie
 
Niliwahi kusema bila kufukuza Kazi hao mameneja wa Mikoa na kuwapa targets reasonable hao TRA watakyangusha Sana.

Afu ifike mahala Utumishi wa umma uwe ni Kazi za mkataba ,mbona private sector wanaweza? Hii kuwapa watu ensurance huku hawafanyi Kazi ni upuuzi
Hivi unajua namna kauli za Samia zilivyovuruga makusanyo ya kodi? Samia kawapa jeuri wafanyabiashara nyakati za kuongea lugha moja zaja, Samia misses integrity and ethics, TRA iko ndani ya uwezo wake alishindwa nini kuitisha kikao na mameneja wote kisha akatoa maelekezo na kusikiliza kero zao. Vituo vya mafuta na biashara zingine za wakubwa kodi bye bye.
 
Wewe unamsumbua tu mama; hasa na hiyo ya kumwita "Rais Wako", mwishowe atadhani anakufanyia kazi wewe!

Mama yupo 'bize', anarekebisha mambo atakavyo yeye yawe.

Unajuaje, labda hao jamaa zako wa TRA wameagizwa kufanya hivyo kuwapa marafiki zake wafanya biashara nafasi ya kupumua, halafu wewe unakuja hapa na kulialia!

Hao rafiki zake wafanya biashara hawatamwacha adondoke. Kama kutakuwepo na wa kudondoka, ni makapuku kama wewe msiojitambua.

Sasa najua hutapenda sana bandiko hili, lakini nadhani ndilo linalokufaa mtu kama wewe, kama nimekusoma vizuri na kukuelewa kwenye bandiko lako hilo!
Samia ana marafiki gani ishu ya kodi na makusanyo yake kazingua sana na itamzingua mwenyewe. Mtake msitake kazingua kodi ndio uhai na heshima ya serikali. Mkisifia sifia ila ukweli kuhusu kodi ni kituko.
 
Ni kama ina ukweli vile; kuna mtu just 30 minutes ago kaniomba ruhusa hivi, "boss samahani, nimekua nafatilia leseni yangu kwa siku 3 sasa TRA, TRA wanasema mtandao wao haufanyi kazi labda leo, nakuomba tafadhari kama masaa 2 au 3 nitakua nimerudi"

Hivi watendaji wa serikali huaga wanataka nini?
 
Sio uongo ni kweli tafuteni taarifa hilo ni kweli bila mtandao TRA haifanyi kazi.
 
Bandiko zuri lakini umekoaea kitu kimoja! Unataka mama alinganishe na mapato ya kodi kipindi cha awamu ya NNE kama kipimo cha kukusanya kodi? Awamu ya NNE wafanyabiashara walipiga sana! Unakumbuka enzi za Home shopping centre!! Leo iko wapi? Makusanyo yalikuwa hayafiki trilioni!! Tusirudi tena kwenye mabilioni! Kimya kimgi kina mshindo mkuu, kwa ninj TRA wameacha kutangaza makusanyo ya kodi? Bila shaka tunapigwa!
Sasa mkuu hizo trillion unajua zimefikaje? Kwenye ukusanyaji bora jk maana hakuingilia mapato ya serikali za mitaa yeye alibaki na mapato yake tu ya serikali kuu homeshoping yeye alisingiziwa sana yaani walikuza vitu vikubwa visivyokuwepo haya sasa leo kaja silent ocean bado anawaibia?
 
Rais wangu, ukipata nafasi mwite ofsini Kamishna wa TRA nchini, Bwana Alphayo Kidata. Muulize katika mwezi April/May ambao yeye amekua ofisini amekusanya mapato kiasi gani. Akikupa hesabu linganisha na mwezi wowote katika mwaka wowote unaoutaka wewe. Achana na miaka ya JPM ambayo inasemwa kodi zilikusanywa kwa nguvu. Tumia mwezi wowote katika kipindi cha awamu ya nne kwa makadilio. Ukipata majibu, mpe nafasi ya mwisho Alphayo Kidata, aache kukuchezea!!

Rais wangu, TRA ya Tanzania haikusanyi kodi tena. Wanafika ofsini kwa muda, wanakaa kidogo katika meza zao zilizopangwa shaghalabaghala, wengine wanawasha kompyuta wengine hawawashi. Baada ya muda mfupi, wanakusanyana nusu yao wanaondoka. Wao wanasema wanakwenda kufanya kazi za nje. Ndugu Rais, TRA ya Tanzania inafanya kazi za nje kwa ajili ya kazi za ndani zisizokuwepo.

Rais wangu, wakati wote huu wote waliobaki ofsini, hawana cha kufanya. Waranda-randa ofsini na kupiga miayo na soga. Wengine wanasimulia habari za msiba wa JPM. Hakuna lolote linalofanyika kwa sababu hakuna mtandao. TRA hawakusanyi pesa kwa sababu ya mtandao, nchi haikusanyi mapato kwa sababu ya mtandao. Tatizo la mtandao wa TRA limekua sugu katika nchi yetu, linajirudia leo, kesho na keshokutwa. No one cares!! Mtu mmoja ameniambia kuwa jana (May, 26) TRA nchi nzima haikufanya kazi. Yaani kwamba, kwa siku nzima nchi yote haikukusanya mapato kupitia chombo chake kikuu cha makusanyo. Kama taarifa hii ni ya kweli basi tatizo ni kubwa. Nchi hii siku hizi haikusanyi pesa, halafu inatumia pesa zilizokusanywa na wengine. Wenye hofu wanasema zikiisha zilizokusanywa nchi inaweza kuanguka.

Rais wangu, nenda leo TRA Mwenge, TRA Tegeta na TRA Kimara (zote za Da'slama), kwa kuzitaja chache. Ukikuta zote zinafanya kazi na inaonesha zimefanya kazi yake ipasavyo kwa siku tatu nyuma au na zaidi, niwajibishe mimi kwa namna utakayoona inafaa. Tuna tatizo kubwa, katika nchi kubwa namna hii kushindwa kukudanya mapato kwa sababu ya mtandao ni aibu. Huu utaratibu usipoangaliwa, nchi itatufia mikononi. Nchi isiyokuwa na mapato yake haiwezi kulipa mishahara kwa wakati, haiwezi kununua dawa za hospitali, hakwezi kugharamia elimu bila malipo na haitoweza kukamilisha miradi ya maendeleo ya gharama kubwa. Tukiruhusu nchi ifike hapo, ndio tumekwenda na maji tayari.

Rais wangu, juzi mtandao wa Tanesco ulisumbua kidogo katika kununua LUKU. Licha ya taarifa iliyotolewa mapema na Tanesco ya kuomba radhi lakini nchi nzima ilisimama. Waziri wa Nishati akahamaki, akafukuza watu hovyo, Waziri Mkuu akasimama kutoa maelekezo. Baada ya muda mfupi, umeme ukarudi. Tanesco haikusanyi mapato kama TRA lakini tuliwekeza nguvu kubwa usiku na mchana. Mtandao wa TRA hauna uhakika kwa zaidi ya mwezi, unasumbua kila siku lakini hakuna anayejali, Waziri wa fedha hajulikani alipo wala hajali.

Rais wangu, ni kama wote tumeridhika na hali hii. Pesa hazikusanywi kwa wakati kwa sababu ya mtandao, watu wanakwenda TRA na kurudi kila siku halafu muda wa kulipa ukipita mfanyabiashara anatozwa faini (penalty) kwa kuchelewa kulipa kodi. Hivi ndivyo tunavyohuisha bishara na kuvutia wawekezaji katika nchi yetu. Mtu kwenda TRA kulipa kodi moja kila siku ni kero, tunaharibu ratiba za watu bila sabbau. Wanaomkumbuka Magufuli wanamkumbuka kwa mengi, sisi tuendelee kufanya kazi za nje tukirudi ndani nchi itakua hoi bin taaban. Rais wangu, TRA watakukwamisha ukiweza chukua hatua sasa

MenukaJr,
Da'slama-Tanzania.
TRA ni tatizo sana Katika nchi hii, wafanyakazi wake wanajua kubambikia watu kodi tu, Sheria za kodi hawajui au wanafanya makusudi, ukienda kuuliza na wao wanaanza kuulizana alafu wanatoa majibu ya mtaani, ukiwambia wakuandikie hayo majibu na wapige mhuri hawataki. yaani wanafanya kazi kama ya babu zao. Kama Raisi asipofanyia kazi TRA itasababisha matatizo makubwa sana na Nia njema ya Raisi ya kukuza uchumi na kuondoa umasikini haitafanikiwa.
 
Mimi nalia na makadirio yao tu ya kodi, unapotaka kuanzisha biashara. Site hawafiki, wanaingia tu kwenye kompyuta zao na kuja na makadirio yao!

Nawashauri siku za usoni, wawe na watu rasmi wa kuzungukia wafanyabiashara, na hasa wale wapya ili kuwatendea haki.
Acha majungu! Unataka TRA waje site gani ambako hakuna hata hiyo biashara yenyewe? Unasema "unapotaka kuanzisha biashara" hii maana yake si huna biashara? Hicho wanachofanya TRA ndio sheria, lia na wabunge wako!
 
Sasa majungu yako wapi hapo! Mimi nimetoa tu maoni yangu na tena nimeshauri! Au umeona nimemtaja mtu, zaidi ya kuitaja hiyo Taasisi? Uwe una akili hata kidogo basi.
 
OP. Mwanzisha thread kazungumzia jambo nyeti sana. Wewe unalalamikia tatizo jingine. Out of Point!
Form six mna akili ndogo sana. Kwani hilo tatizo analo zungumzia mtoa mada linamuongelea babu yako, au linazungumzia TRA? Unafahamu maana ya OP wewe?
 
Back
Top Bottom