Rais Samia, kama ulivyofanya kwenye vyumba vya madarasa, fanya kwenye Umeme Vijijini

tinkanyarwele

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2016
Posts
2,016
Reaction score
1,946
Kwako Mh Rais Samia Suluhu Hassan,

Slaam Mh Rais, NAKUSALIMIA KWA JINA LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA. Binafsi nikupongeze kwa kazi kubwa sana na ya kipekee sana ya kusukuma mbele gurudumu la maendeleo kwa ajili ya Tanzania na watanzania, Mh Rais binafsi nikupongeze pia kwa kazi nzuri ya kuongeza vyumba vya madarasa katika shule zote Tanzania zilizokuwa na uhitaji, hakika kwa hili umeandika historia ya kipekee ambayo haitafutika pia.

Mh Rais, nijikite kwenye suala la umeme vijijini chini ya REA, ki ukweli tunatambua nia ya dhati ya serikali ya Tanzania ya kuwafikishia huduma ya umeme wananchi wa vijijini na kila muungwana wa Taifa hili lazima akubaliane na mimi kuwa umeme ni chachu kubwa sana ya maendeleo.

Ukweli ni kwamba tunaambiwa kuwa vimebaki kama vijiji elf 3..kati ya vijiji elf 12 ambavyo bado havijafikiwa na huduma ya umeme, lakini ukweli ni kwamba bado wananchi wengi sana hawana umeme, kilichofanyika na kinachofanyika tu ni kufikisha umeme kwenye kijiji ( haswa maeneo muhimu km hospitali, shule au kwa wenye uzito kidogo) kisha kuhesabu kuwa tayari kuna umeme, mfano unakuta kijiji kina vitongoji sita lakini umeme inaingizwa kwenye kitongoji kimoja tu! Vitongoji vinne vinabaki bila umeme, na bado unakuta raia ambao wamesalia bila umeme hawana uwezo wa kuvuta umeme kutoka kitongoji jirani! Baya zaidi, takwimu zinaandikwa kuwa maeneo hayo yana umeme tayari, hali hii imepelekea asilimia kubwa sana ya Watanzania kubaki bila umeme vijijini.

Nakuomba sana Mh Rais km itakupendeza ufanye jitihada binafsi za kupata hata fungu lielekezwe kwenye umeme vijijini ikiwezekana kila KITONGOJI kiwe na umeme, na kama kutakuwepo vitongoji ambavyo huduma haiwezi kufika kwa urahisi basi wananchi wa eneo hilo wapatiwe huduma mbadala ya nishati mfano Umeme wa Jua.

Mh rais, yaani kasi ambayo imetumika kwenye kuongeza vyumba vya madarasa( nakupongeza sana kwa hili pia) basi itumike kwenye kusambaza umeme VITONGOJINI vilevile.

Mh Rais, vilevile ingependeza kauli za kusema kuwa umeme kila KIJIJI ifutwe iwe umeme kila KITONGOJI na hatimaye tutaenda umeme kila NYUMBA.

Mh Rais, ingependeza siasa ziwekwe pembeni kwenye suala la maendeleo, takwimu ambazo si sahihi zisitolewe bali zitolewazo ziwe sahihi, na njia ya kukwepa hali hii ni kuanzisha mfumo ambao utakuwa unaonesha mkoa, wilaya, tarafa, kata kijiji na kitongoji kipi kimepata huduma ya umeme na kipi hakijapata huduma hiyo.

Na iwe wazi kila mtanzania aweze kuingia na kuona muda wowote.

Vilevile bei ya umeme wa REA ambayo ni 27,000/= bado haimfanyi mteja kupata umeme (japo inawezekana lakini ni ngumu) basi kama serikali imeelemewa kwa hili, wananchi tuko tayari hata kuchangia la msingi Watanzania woote tufurahi pamoja na tujumuike pamoja kujenga taifa letu wote vitongojini kuwe na huduma nyeti hii ya umeme. Mh Rais tukumbuke kwamba umeme unafaida kubwa sana mfano

1) Vijana wataweza kujiajiri huko vitongojini
2) Makaazi ya watu yatakuwa bora zaidi
3) Watu wanaweza kupunguza kukimbilia mijini wakabaki vijijini pia ( hata baadhi ya watumishi wa umma hukwepa sana kufanyia kazi kwenye maeneo yasiyo na umeme)
4) Kuongeza ufahulu na kukuza taaluma kwa watoto wetu maana na wao watapata muda wa kujisomea hata usiku,( kumbuka watoto wengi wa shule za msingi na za sekondari za kata huishi vijijini ambako hakuna umeme hivyo wakipata umeme itakuwa vyema kabisa na yamkini wakaanza kufanya vizuri ki masomo kuliko hata wale wa mijini
5) Ulinzi na Usalama vitongojini utaongezeka kiasi chake
6) Wananchi wataongeza muda wa kufanya kazi maana hata usiku kuna kazi zitafanyika kwa urahisi kama kuna Mwanga wa kutosha
7) Viwanda vidogovidogo vitaongezeka huko vitongojini maana umeme utachochea shughuli mbalimbali
8) Burudani zitaongezeka pia na hii itachangia kupunguza misongo ya mawazo na kurefusha muda wa kuishi
9) Huduma za jamii km maji ni rahisi sana kupatikana km watu watapata umeme, huduma za jamii km saluni nk zitaongezeka pia.
10) Kupunguza gharama za maisha, mfano kununua au kutunza hata vyakula vya ziada kwenye majokofu ni
11.... faida ziko nyingi sana

Ikiwezekana hili suala la umeme vijijini/ vitongojini liwe ni AJENDA YA KITAIFA.

Mwisho, km haya yatashindikana basi tusaidie kurahisishiwa kwenye taratibu za kupata umeme maana ukweli ni kwamba Tanzania hii mtu kupata huduma ya umeme ni mchakato mgumu sana sana tena sana...lakini kwa kutaka ukweli wa hili basi Mh Rais na mawaziri husika chunguza kwa chini chini mtajua ni kwa kiasi gani huduma ya kupata umeme ilivyo ngumu si kawaida.

Mh Rais, binafsi natamani sana kuona hili likifanyika kwa Taifa zima na naamini kwa jitihada zako hii inawezekana. Nakutakia maisha marefu na utendaji mwema uliotukuka. Pia...iende kwa waheshimiwa

i) Januari Makamba (W. NISHATI)
ii) Steven Byabato (NW NISHATI)
iii) Ummy Mwalimu (TAMISEMI)
iv) Mwigulu Mchemba (W.FEDHa)
v) Job Y Ndugai ( Spk. BUNGE)
 
Vijijin umeme inahesabiwa kama wanafanyiwa fadhira.

Hata barabara za lami Mbeya Kama sio sehemu ya mapato nchi hii.
 
Hoja yako imejibiwa Leo na Mh.RAIS umepigwa na kitu kizito kichwani
 
Back
Top Bottom