Rais Samia kapata wapi ujasiri wa kusafiri ilhali kuna majanga nchini?

Halafu ati bila aibu ana hutubia Taifa kuhusu hili janga la Kariakoo akiwa Brazil. Ccm mna shida sana. Mna tupenda kipindi cha uchaguzi tuu. Hongereni. Tuta kapo amka myie mta lala
 
Kwani hao waathirika wana undugu na wàtanzania wote hadi kila mtu akose nguvu za kuendelea na mambo yake? Acheni kukuza mambo mengine hayahusu kila mtu.
 
Nimekuelewa ndugu yangu..Ila Kama taifa tunakauzito Fulani kukabiliana na majanga..

Mfano Leo maeneo ya msikitini njia ya mbagala majira ya mchana gari IST imewaka kiasi Cha kuteketea kubakia bodi
Baada ya muda ndio Zima moto imekujaa kumwaga maji

Kama una ndugu pia wadau walio pita hapo majira ya mchana wata toa testimony

Tupo nyuma Sana wandugu let say upate janga la kuumwa au dharula UNAKUFA KIZEMBE KABISA TANZANIA tunaishi kwa kudra za MUNGU.
 
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO
 

Attachments

  • IMG-20241117-WA0032.jpg
    118.5 KB · Views: 6
Acha kuleta siasa kwenye uhai wa watu.
 
Mleta mada wewe kaa tu ulie lie. Rais wa nchi anategemewa na watu milioni 60, na pia nchi nyingi za jirani zinategemea Tanzania kwa baadhi ya huduma, usalama, biashara, usafiri n.k.
Kwa hiyo rais ana majukumu mapana na marefu na ni lazima awe imara kisaikoligia asitetereke kwenye changamoto au majanga sababu uamuzi wake ndio ufunguo na suluhisho.
Hapo wakati wewe Bado unakua rais zamani aliisha kaa na wahusika, .kuchambua kilichotokea na kutoka maelekezo ya kufanya jitihada za uokozi ukifuatiwa kila dakika na uongozi wa juu serikalini.
Tupunguze mihemko na kutaka kutumia
majanga kisiasa.
 


Raisi anakula bata na tutasubiri ripoti za polisi fake kama zile za utekaji 😂. Huyu ndiye Mama bwana. Ni yeye na familia yake tu basi
 
Raisi anakula bata na tutasubiri ripoti za polisi fake kama zile za utekaji 😂. Huyu ndiye Mama bwana. Ni yeye na familia yake tu basi
Gentleman,
naona unachanganya mambo huku ukiwa na furaha kweli kweli, hali ya kua kuna maafa. Kulikoni gentleman? 🐒
 
Gentleman,
naona unachanganya mambo huku ukiwa na furaha kweli kweli, hali ya kua kuna maafa. Kulikoni gentleman? 🐒


Mama yenu anakula bata msipotoshe na hakuna mtu atafukuzwa watanzania wakifa. Nyie mnanunua washawasha kwa chadema tu yaani Polisi wamepewa na Mama bilioni 100 za magari ya washawasha na kukabiliani na wapinzani lakini ni lini mtu kafukuzwa kwenye serikali hii kwa uzembe kama huu wa kariakoo mtaishia kulaumu Chadema. Tumesema haya kwa miaka mingi nyie machawa mnatetea kila kitu sasa walikufa huko ni chadema? Kuna tofauti na uchawa na uzalendo
 
Afadhalli utoe upotofu moyoni mwako ili angalau upate relief gentleman na itapendeza zaidi.

Cha muhimu zaidi kuzingati ni kwamba mihemko na makasiriko miongoni mwa viongozi waandamizi wa Chadema wanaolumbana ni kwa maslahi yao.

CCM iko kwajili ya maslahi mapana ya waTanzania na una jukumu muhimu la kuwatumikia wanainchi, haiwezi hata siku moja, kubabaika na mbambamba za mtu awaye yeyote mwenye mihemko yake 🐒
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo
 

Attachments

  • IMG-20241117-WA0032.jpg
    118.5 KB · Views: 5
Halafu ati bila aibu ana hutubia Taifa kuhusu hili janga la Kariakoo akiwa Brazil. Ccm mna shida sana. Mna tupenda kipindi cha uchaguzi tuu. Hongereni. Tuta kapo amka myie mta lala
Alitakiwa arudi hata akatishe safari hiyo kwani uhai wa binadamu ni muhimu zaidi ya mkutano huo
 

Sawa endelea kushabikia na uchawa Serikali inafanya kazi nzuri sana tuna vifaa vya ukoaji, majengo yanakaguliwa kama sheria inavyofanya na tuna demokrasia basi furahi na endeleo na maisha yako fake kama ndiyo unavyofikiria.

Sisi wengine tutaendelea kurekebisha kutaka demokrasia, katiba, usalama kweli wa raia kama kariakoo na sio washawasha na kujali nchi na sio chama chochote. Wewe endelea na uchawa wako na sisi tunaendelea na mapambano ya taifa hili. Kila mtu ana wito wake.
 
Serikali sikivu ya CCM haiwezi kubabaika na makasiriko wala mihemko ya kibaraka au mercenaries wao wowote humu nchini..

kwasasa,
Serikali iko kazini kuhakikisha wahanga wote waliokwama kwenye vifusi kwenye jengo lililoporomoka kariokoo wanaopolewa kadiri iwezekanavyo..

Pamoja na hayo,
kazi ya kuwatumikia waTanzania haijasimama, bali unaendelea kwa kasi, bidii na weledi wa kiwango cha juu sana.

Inshallah,
Kwa Neema na Baraka za Mungu, Rais na kipenzi cha waTanzania wote Dr. Samia suluhu Hassan atapewa muhula mwingine wa pili kuanzia October 2025.

Asanti sana waTanzania wote kwa uamuzi huo wa kishujaa, kijasiri na wa kizalendo. Mitano tena kwa Dr Samia suluhu Hassan 🌹
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…