Rais Samia: Kodi ndio Damu ya Serikali

Rais Samia: Kodi ndio Damu ya Serikali

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Ndugu zangu Watanzania,

Rais wetu Mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan kwa uchungu,hisia kali na msisitizo mkali sana.amesema ya kuwa Kodi ndio Damu ya serikali.ambapo kila Mtanzania anapaswa kulipa kodi.

Hii maana yake nini watanzania wenzangu? Hii ni katika kuwakumbusha watanzania wajibu wao au wetu sote katika ujenzi wa Taifa letu. Maana yake ni kuwa watanzania ni lazima tujisikie fahari kulipa kodi kwa hiyari ya mioyo yetu.tukitaka maendeleo ya aina yoyote ile ni lazima tuwajibike kulipa kodi bila kutafuta chochoro za kukwepa kodi.

Ni ulipaji wa kodi stahiki utafanya serikali yetu kuwa na uwezo wa kujenga zahanati na vituo vya afya vya kutosha.kuajiri watumishi wa afya wa kutosha na katika ngazi zote,kununua vifaa tiba na madawa ya kutosha na ya kila ugonjwa. Kujenga na kuboresha ama kukarabati shule ,kuongeza vyumba vya madarasa ili kuendana na ongezeko la wanafunzi,kuajiri walimu wa masomo yote pamoja na kuwa na maabara za kisasa kwa masomo yote ya sayansi.

Ni ulipaji kodi stahiki utakao iwezesha serikali yetu kuwa na uwezo wa kujenga miundombinu ya barabara, usambazaji wa maji safi na salama,upandishaji wa mishahara kwa watumishi wa umma ili kuwaongezea morali ya kazi na kumudu gharama za Maisha,ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo pia itatoa fursa mbalimbali za ajira kwa vijana pamoja na kuchochea mzunguko wa fedha mitaani na biashara kushamiri.

Sasa huwa inashangaza unakuta mfanyabiashara au mtu ni mkwepa kodi mkubwa lakini huyo huyo analalamika juu ya ubovu wa huduma fulani ya serikali.bila kujua kuwa serikali haina pesa ila wananchi ndio wenye pesa na tunaopaswa kuchanga kupitia mfumo wa kodi ili serikali ilete na kusambaza huduma kwa wananchi.

Kwa hiyo ni wajibu wetu wananchi kumuunga mkono Rais wetu kwa kulipa kodi bila kukwepa.hata Mataifa yaliyoendelea yamefika hapo yalipo kutokana na ulipaji wa kodi.Nchi za wenzetu ni wakali na wachungu sana linapokuja suala la ulipaji kodi.na ni kosa kubwa sana ikibainika wewe ni mkwepa kodi au umewahi kukwepa kulipa kodi mwaka fulani katika biashara fulani au kitu fulani.

Ndio maana ni kawaida sana kuona wachezaji wakubwa wenye majina makubwa ulaya wakiburuzwa mahakamani bila kujali ukubwa na umaarufu wa majina yao kwa makosa ya ukwepaji kodi.wenzetu walishajuwa kuwa kodi ndio moyo na kitovu cha maendeleo ya Nchi na ni Damu iendeshayo serikali kama alivyosema Mama yetu Mpendwa Daktari Samia Suluhu Hasssan.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Pia soma:Rais Samia: Uchumi wetu unakua lakini tunachokusanya, kingi kinaingia mifukoni kwa Watu
 
Kaka Luka unadhani kodi kulipa ni tatizo ndugu yangu, kinachouma ni kuona matumizi mabaya ya hiyo kodi na ufisadi kwenye hizo kodi!

Hapo tu ndio mambo yanapogongana
Naamini Mheshimiwa Rais analitambua hilo na ndio maana amelisema hadharani.hiyo ikimaanisha kuwa hatua kali zitachukuliwa kwa wahusika ili kila senti inayokusanywa ifike mahali husika na ifanye kazi ya maendeleo na yenye kugusa maisha ya watanzania
 
images.jpeg
 
Na je ili kupata damu ya kutosha kuendesha mwili wa serekali vizuri kwanini tusilipe wote kodi, kwanini wabunge, wanasiasa, yeye mwenyewe MAma yetu mpendwa nao wasilipe kodi?

Hivi Luka, ni sawa kwa mwalimu wa grade A kijijini huko au kijana mfanyabiashara wa kisaluni sebuleni kwa baba yake kulipa kodi kisha wabunge hawalipi? Hawa wenzetu waheshimiwa damu yao ni type gani isiyochangamana na magroup mengine kuendesha serekali?
 
Na je ili kupata damu ya kutosha kuendesha mwili wa serekali vizuri kwanini tusilipe wote kodi, kwanini wabunge, wanasiasa, yeye mwenyewe MAma yetu mpendwa nao wasilipe kodi?

Hivi Luka, ni sawa kwa mwalimu wa grade A kijijini huko au kijana mfanyabiashara wa kisaluni sebuleni kwa baba yake kulipa kodi kisha wabunge hawalipi? Hawa wenzetu waheshimiwa damu yao ni type gani isiyochangamana na magroup mengine kuendesha serekali?
Nadhani hilo ni suala la mjadala mwingine linalopaswa kuzirejea sheria zetu ili kila mtu alipe kodi kwa kila pesa aipatayo kama mapato kwa kufanya shughuli fulani inayomuingizia kipato
 
Nadhani hilo ni suala la mjadala mwingine linalopaswa kuzirejea sheria zetu ili kila mtu alipe kodi kwa kila pesa aipatayo kama mapato kwa kufanya shughuli fulani inayomuingizia kipato
Nawaza hili lingetangulia bro.

Watu wanakatishwa tamaa kuona wao ndio walipa kodi kuendesha uchumi alafu wabunge hawalipi kodi na wananunuliwa ma V8 kwa kodi ile ile wanayolipa waalimu.

Inauma Lukas! Inauma bro!
 
Nawaza hili lingetangulia bro.

Watu wanakatishwa tamaa kuona wao ndio walipa kodi kuendesha uchumi alafu wabunge hawalipi kodi na wananunuliwa ma V8 kwa kodi ile ile wanayolipa waalimu.

Inauma Lukas! Inauma bro!
Ni suala la kurekebisha sheria zetu.maana hilo lipo kisheria. Lakini kumbuka pia sheria zote zinatungwa na Bunge.
 
Back
Top Bottom