Rais Samia: Kodi ndio Damu ya Serikali

Rais Samia: Kodi ndio Damu ya Serikali

Ni suala la kurekebisha sheria zetu.maana hilo lipo kisheria. Lakini kumbuka pia sheria zote zinatungwa na Bunge.
Kwahiyo wabunge wanajitungia sheria wao wasilipe na sisi tulipe ilhali wao wanatumia sehemu kubwa ya keki ya Taifa ipatikanayo kwa kodi hizo?

Unakwepa tu blaza kukubali, kubali tatizo lipo na halishawishi kulipa kodi!
 
Mimi silipwi kwa ajili ya kuandika hapa jukwaani
Hivi ni kwa nini hili suala nimekuwa nikilisikia hivyo hivyo miaka yote mimi nilitegemea kuwa mwaka huu nitasikia kuwa walipa kodi wamefikia milioni 7 au nitatizo limeshindikana!?
Nilitegemea baada ya kuwa na makamu wa rais mchumi waziri wa fedha mchumi dalaja la kwanza basi mambo yatabadilika lakini mambo ni yaleyale.
Kuna nini!?
 
Kuna direct tax na indirect tax. Direct tax inahitaji mambo mengi sana kuongeza walipakodi wa kundi hilo.ikiwepo sera,sheria na Mambo mengine mengi
 
Ndio sasa si tunaiweka serikali madalakani ili ishughulikie hayo mambo sasa wanashindwa nini wimbo ni huo tangia utawala wa mkapa mpaka sasa malalamiko ni yaleyale
 
Ndugu zangu Watanzania,

Rais wetu Mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan kwa uchungu,hisia kali na msisitizo mkali sana.amesema ya kuwa Kodi ndio Damu ya serikali.ambapo kila Mtanzania anapaswa kulipa kodi.

Hii maana yake nini watanzania wenzangu? Hii ni katika kuwakumbusha watanzania wajibu wao au wetu sote katika ujenzi wa Taifa letu. Maana yake ni kuwa watanzania ni lazima tujisikie fahari kulipa kodi kwa hiyari ya mioyo yetu.tukitaka maendeleo ya aina yoyote ile ni lazima tuwajibike kulipa kodi bila kutafuta chochoro za kukwepa kodi.

Ni ulipaji wa kodi stahiki utafanya serikali yetu kuwa na uwezo wa kujenga zahanati na vituo vya afya vya kutosha.kuajiri watumishi wa afya wa kutosha na katika ngazi zote,kununua vifaa tiba na madawa ya kutosha na ya kila ugonjwa. Kujenga na kuboresha ama kukarabati shule ,kuongeza vyumba vya madarasa ili kuendana na ongezeko la wanafunzi,kuajiri walimu wa masomo yote pamoja na kuwa na maabara za kisasa kwa masomo yote ya sayansi.

Ni ulipaji kodi stahiki utakao iwezesha serikali yetu kuwa na uwezo wa kujenga miundombinu ya barabara, usambazaji wa maji safi na salama,upandishaji wa mishahara kwa watumishi wa umma ili kuwaongezea morali ya kazi na kumudu gharama za Maisha,ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo pia itatoa fursa mbalimbali za ajira kwa vijana pamoja na kuchochea mzunguko wa fedha mitaani na biashara kushamiri.

Sasa huwa inashangaza unakuta mfanyabiashara au mtu ni mkwepa kodi mkubwa lakini huyo huyo analalamika juu ya ubovu wa huduma fulani ya serikali.bila kujua kuwa serikali haina pesa ila wananchi ndio wenye pesa na tunaopaswa kuchanga kupitia mfumo wa kodi ili serikali ilete na kusambaza huduma kwa wananchi.

Kwa hiyo ni wajibu wetu wananchi kumuunga mkono Rais wetu kwa kulipa kodi bila kukwepa.hata Mataifa yaliyoendelea yamefika hapo yalipo kutokana na ulipaji wa kodi.Nchi za wenzetu ni wakali na wachungu sana linapokuja suala la ulipaji kodi.na ni kosa kubwa sana ikibainika wewe ni mkwepa kodi au umewahi kukwepa kulipa kodi mwaka fulani katika biashara fulani au kitu fulani.

Ndio maana ni kawaida sana kuona wachezaji wakubwa wenye majina makubwa ulaya wakiburuzwa mahakamani bila kujali ukubwa na umaarufu wa majina yao kwa makosa ya ukwepaji kodi.wenzetu walishajuwa kuwa kodi ndio moyo na kitovu cha maendeleo ya Nchi na ni Damu iendeshayo serikali kama alivyosema Mama yetu Mpendwa Daktari Samia Suluhu Hasssan.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.

Kila mtu anataka kulipa Kodi

Ukakasi unakuja pale Tu unapolipa Kodi ya Jasho lako then anaenda kupewa mtu Kwa ajili ya kuandika Tu kwenye mitandao Sifa za Rais
 
Kwani huyo samia zile saa zake za milioni 600 vipi zimehalibia au anataka hela kununua zingine ...nani alipe kodi hili viongozi wahuni mzidi kujinenepesha kwa kodi zetu.
 
Wewe ni mpotoshaji na Mzushi sana.

Hiyo ndio sababu watu hawataki kulipa Kodi

Hata Rais akasema Leo, pesa zinaishia kwenye Mifuko ya watu

Kauli hii angesema mbowe ungekuja fasta kutetea na kusema si kweli mama ameweka mifumo mzuri

Haya sasa kasema mwenyewe eeh unasemaje ? Huna la kusema

Kodi ya kupigwa na jua kariakoo then kuna mtu analipwa akiwa amekaa na laptop yake kazi yake ni kusema Tu mama mitano tena

It's very painful
 
Kwani huyo samia zile saa zake za milioni 600 vipi zimehalibia au anataka hela kununua zingine ...nani alipe kodi hili viongozi wahuni mzidi kujinenepesha kwa kodi zetu.
Ulilipia wewe hiyo saa ya millioni mia 6? Au unajiongelea tu kama mtoto mdogo
 
Back
Top Bottom