Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajia kusafiri kuelekea Harare, Zimbabwe kesho tarehe 31 Januari, 2025 kwa ziara ya kikazi ya siku moja.
Akiwa nchini Zimbabwe, Rais Dkt. Samia atashiriki Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC ulioitishwa kwa lengo la kujadili hali ya ulinzi na usalama Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Mkutano huo utaongozwa na Mhe. Dkt. Emmerson Dambudzo Mnangagwa, Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe na Mwenyekiti wa SADC.
Mkutano huo unafanyika kufuatia Mkutano wa Dharura wa Utatu wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama (SADC Organ Troika), nchi zinazochangia askari katika Misheni ya SADC nchini DRC (SAMIDRC), uliofanyika tarehe 28 Januari, 2025 na kuongozwa na Mwenyekiti wa Asasi hiyo Mhe. Rais Dkt. Samia.
Sharifa B. Nyanga
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu