Rais Samia kufanya Ziara ya Kihistoria Mkoani Katavi Julai 12-15, 2024

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Ndugu zangu Watanzania,

Ni historia,ni furaha na tabasamu,ni heka heka na chereko,ni shauku na kiu kubwa sana iliyojaa katika mioyo ya wana Katavi ambao wameripuka kwa shangwe ,nderemo na vifijo baada ya kupata taarifa ya ugeni mzito na wa kihistoria ya Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan.ambaye anakwenda kuanza na kufanya ziara kuanzia Tarehe 12-15 Mwezi huu.

Mkoa mzima wananchi wanatamani wafagie njia na barabara zote atakazopita Mama yao,wanaona ni baraka na neema kubwa sana kwa Mama kukanyaga ardhi ya Katavi, wanajuwa neema inakwenda kushuka.wana kiu ya kumuona mama ana kwa ana ,wana taka waseme asante mama kwa upendo wako kwa wana Katavi ambao wamepelekewa miradi mbalimbali ya maendeleo kuanzia barabara,umeme,Elimu,afya n.k.

Wanataka wakamhakikishie kumpatia kura za ndio kwa kishindo na kumuomba achukue Fomu ya Urais hapo Mwakani.wanataka akajionee Mwenyewe namna wanavyomuunga mkono kwa kuchapa kazi usiku na mchana kulijenga Taifa lao. Wana Katavi wana imani kubwa sana na Rais Samia na wana furaha kubwa sana kuona akitua katika mkoa wao.

Watendaji wa serikali kaeni mkao wa kula maana atakayebainika kukwamisha juhudi za Mheshimiwa Rais katika kuwahudumia wananchi,basi ajuwe kuwa atakwenda na maji.nazani mnakumbuka alipofanya ziara kule kusini namna alivyopangua na kufanya utenguzi kikomandoo.kumbukeni Rais wetu hanaga uvumilivu wala subira ya kumvumilia mzembe,mvivu,goigoi na mtu anayetaka kusukumwa sukumwa tu katika kazi.yeye kazi yake ni kucheza na kalamu tu.

Kwa hiyo nawatahadhalisheni watumishi wa umma wazembe na mliokuwa mnajifanya miungu watu na msiogusika.sasa Mama wa Taifa anakuja huko, komandoo wa vita anatua huko,shujaa wa Afrika anapiga hodi huko,Simba wa Nyika anakuja kutikisa na kutetemesha huko mpaka wanyama mbuga ya Katavi wasimame wima kupisha kishindo kitulie.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa.Mama anatosha kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Lucas ulivyopotea nimepokea simu nyingi sana za wana jukwaa kukuulizia
Nikawajibu umekata tamaa ya kua chawa,
kumbe bado unaendelea na kazi, ulienda kutia mwili nguvu mpya

Mwaka huu teuzi tunayo au hatuna?
 
😀😀😀Mimi nipo ephen wangu
 
Lucas ulivyopotea nimepokea simu nyingi sana za wana jukwaa kukuulizia
Nikawajibu umekata tamaa ya kua chawa,
kumbe bado unaendelea na kazi, ulienda kutia mwili nguvu mpya

Mwaka huu teuzi tunayo au hatuna?
Dah yaan una uma na kupuliza ila wewe🤣🤣🤣.Acha nisome hiyo ziara ilivyo nibubujukwe na machozi mapema.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Ni historia,ni furaha na tabasamu,ni heka heka na chereko,ni shauku na kiu kubwa sana iliyojaa katika mioyo ya wana Katavi ambao wameripuka kwa shangwe ,nderemo na vifijo baada ya kupata taarifa ya ugeni mzito na wa kihistoria ya Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan.ambaye anakwenda kuanza na kufanya ziara kuanzia Tarehe 12-15 Mwezi huu.

Mkoa mzima wananchi wanatamani wafagie njia na barabara zote atakazopita Mama yao,wanaona ni baraka na neema kubwa sana kwa Mama kukanyaga ardhi ya Katavi,wanajuwa neema inakwenda kushuka.wana kiu ya kumuona mama ana kwa ana ,wana taka waseme asante mama kwa upendo wako kwa wana Katavi ambao wamepelekewa miradi mbalimbali ya maendeleo kuanzia barabara,umeme,Elimu,afya n.k.

Wanataka wakamhakikishie kumpatia kura za ndio kwa kishindo na kumuomba achukue Fomu ya Urais hapo Mwakani.wanataka akajionee Mwenyewe namna wanavyomuunga mkono kwa kuchapa kazi usiku na mchana kulijenga Taifa lao. Wana Katavi wana imani kubwa sana na Rais Samia na wana furaha kubwa sana kuona akitua katika mkoa wao.

Watendaji wa serikali kaeni mkao wa kula maana atakayebainika kukwamisha juhudi za Mheshimiwa Rais katika kuwahudumia wananchi,basi ajuwe kuwa atakwenda na maji.nazani mnakumbuka alipofanya ziara kule kusini namna alivyopangua na kufanya utenguzi kikomandoo.kumbukeni Rais wetu hanaga uvumilivu wala subira ya kumvumilia mzembe,mvivu,goigoi na mtu anayetaka kusukumwa sukumwa tu katika kazi.yeye kazi yake ni kucheza na kalamu tu.

Kwa hiyo nawatahadhalisheni watumishi wa umma wazembe na mliokuwa mnajifanya miungu watu na msiogusika.sasa Mama wa Taifa anakuja huko, komandoo wa vita anatua huko,shujaa wa Afrika anapiga hodi huko,Simba wa Nyika anakuja kutikisa na kutetemesha huko mpaka wanyama mbuga ya Katavi wasimame wima kupisha kishindo kitulie.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa.Mama anatosha kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Tulikukumbuka sana Mzee,Karibu tena. Bila watu kama nyie JF hainogi.
 
Katavi imefunguka, barabara za kuunga mkoa zote lami, uwanja wa ndege safi. Zamani safari ya Katavi ilifanana na ya kuzimu
 
Back
Top Bottom