Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 40,476
- 26,173
Ndugu zangu Watanzania,
Siku ya Kesho ni Siku Ambayo Rais Wetu Mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan anakwenda kuzungumza na Taifa na Dunia nzima kwa ujumla wake.
Ni Siku Ambayo Mama yetu na Rais wetu Mbeba Maono na Moyo Wa Taifa letu anakwenda Kutoa Muelekeo kwa masuala mbalimbali kwa Taifa Kama vile masuala ya wafanyakazi na Maslahi yao,uchumi ,ajira na mambo mengine mengi sana.
Hakuna Jiwe litakalobakia pasipo Kugeuzwa. Hakuna kitu ambacho hakitaguswa,hakuna mtu ataachwa na kiu, hakuna atayebakia kama alivyokuwa awali. Ni Siku ya Matumaini kwa watu wote,ni siku ya Ukurasa Mpya kwa Taifa ,ni Siku ya Mwanzo mwingine wa Matumaini kwa watumishi wa umma.
Ikumbukwe ya kuwa Jemedari wetu kipenzi Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan ndiye kiongozi Mwenye ushawishi zaidi barani Afrika na Duniani kote kwa ujumla wake. Ndio maana amekuwa akipata heshima ya kualikwa katika matukio mbalimbali muhimu kama ambavyo tulishuhudia akialikwa katika mkutano wa Nchi 20 Matajiri zaidi Duniani kule Nchini Brazil.
Lakini pia ni kwa ushawishi wake Barani Afrika na Duniani kote tulishuhudia akipata mualiko katika Uapisho wa Rais wa Namibia na kupewa nafasi ya kutoa hotuba yake. Lakini pia alipewa mualiko kule Angola. Lakini pia Rais wetu alipewa nafasi ya kuwa Makamu mwenyekiti wa Mkutano wa kujadili matumizi ya nishati safi ya kupikia kule Paris Ufaransa.
Nawakumbusheni ya Kuwa Rais Samia ndiye kinara wa kupigania matumizi ya nishati safi ya kupikia Duniani kote . Lakini pia ndiye Mwamba na Nguli anayetambulika na Umoja wa Afrika katika kutokomeza na kupunguza Vifo vya Mama na mtoto Barani Afrika. Ndio maana amekuwa akipewa na kutunukiwa tuzo mbalimbali kutoka maeneo mbalimbali Duniani kama ambavyo tumeshuhudia akipewa heshima hiyo kutoka Nigeria siku chache zilizopita.
Kwa Hiyo ni jambo lisilopingika kuwa huwezi kuizungumzia Afrika bila kumzungumzia Rais Samia na mchango wake katika Mapinduzi ya kiuchumi,kilimo n.k. ni Rais ambaye amegusa kila secta na kuleta matokeo Chanya. Ndio Maana hotuba zake zimekuwa zikifuatiliwa na watu wengi sana Duniani kote. Na amekuwa ni mfano wa Kuigwa kwa uchapakazi wake, uzalendo wake ,umahiri wake kiuongozi na Amefungua milango ya wanawake wengi sana kuwa viongozi na kuaminiwa kushika nafasi kubwa za kiuongozi.
Ewe Mtanzania usikose kufuatilia Hotuba ya Rais wetu Mpendwa siku ya kesho ili usije kujutia baadaye. Usipange kuchelewa ukakuta Rais Ameanza kutoa hotuba yake. Fanya maandalizi yako mapema na ukae mkao wa kupata jambo ambalo hujawahi kupata.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.