Umesamehewa bure kabisa makosa yako maana hujui ulitendalo
Unasamehe kama nani? Na kwa kosa gani?
Wewe unastahili kuomba sana neema ya Mungu ili uijiriwe na hekima ya Mungu upate kukombolewa. Mungu wetu ni Mungu wa haki, ukiona unafurahia dhuluma na mauaji ya binadamu wenzako, ujue kuwa shetani amefanya makao yake ndani ya nafsi yako. Ukiijiriwa na hekima, ukatubu na kuomba msamaha kwa dhamira, Mungu atakusamehe, utarufia kwenye ubinadamu wako na kujitenga na shetani, hutatamani kuwa chawa tena wala hutafurahia dhuluma na mauaji wa wanadamu wenzako, wala hutawashangilia na kuwasifia wauaji, zaidi utawaonya kutokana na uovu wai.
Omba sana neema ya Mungu uondokane na huyo shetani aliweka makao ndani yako, kisha ujutie na kuomva toba ya kweli, na kwa sababu Mungu wetu ni tajiri wa msamaha, atakusamehe, kama anavyosamehe wadhambi wengine.