Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
Rais wetu Mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan. Anatarajiwa kuisimamisha Nchi na Afrika Nzima kwa ujumla wake pamoja na nje ya mipaka ya Bara la Afrika June 27 mwaka huu.
Ni Tarehe ambayo anatarajiwa kutua na kuingia kikomandoo ndani ya Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya kufanya kazi mbili tu. Ambazo ni kulihutubia Bunge na kisha kulivunja Rasmi Bunge la 12.
Hiyo itamaanisha kuwa waheshimiwa wabunge watatakiwa kila mmoja wao kurejea jimboni kwake na kuwakuta wananchi na wajumbe mbalimbali wakiwasubiri kwa hamu kubwa sana kwa ajili ya kuwapa hukumu kila mmoja kwa kadri alivyo fanya kwa miaka 5 iliyopita.
Hapa kutakuwa na vita moja kali sana kuwahi kutokea hapa Nchini hususani ndani ya CCM katika kura za maoni kutoka kwa wajumbe. ambapo sasa wameongezeka zaidi kwa kuwa hadi mabalozi watahusika katika kupiga kura.
Kwa hakika kila mmoja atavuna alichopanda . Hukupanda kitu basi usitarajie kuvuna kitu wala kutumia nguvu kulazimisha kupendwa na kuvuna mazao.
Na mpaka sasa wajumbe wanajua ni nani anapaswa kupewa nafasi ya kuwaongoza na ni nani anapaswa kuliwa kichwa. Mpaka sasa wanajua ni nani amekuwa karibu yao na nani yupo kwa ajili ya kushibisha tumbo lake.
Nawaonea sana huruma wale ambao mmekumbuka mashuka wakati kumekucha. Ninyi ni bora mpokee tu na kutunza viinua mgongo vyenu badala ya kuvipoteza na kuja kukosa hata huo Ubunge wenyewe.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.