PostGE2025 Rais Samia kumuapisha Dkt. Mwigulu Nchemba kuwa Waziri Mkuu kesho Novemba 14, 2025

PostGE2025 Rais Samia kumuapisha Dkt. Mwigulu Nchemba kuwa Waziri Mkuu kesho Novemba 14, 2025

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Mpogole Kusiluka, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan atamuapisha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb.) kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tarehe 14 Novemba, 2025

Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb.) ameteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na jina lake kuthibitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tarehe 13 Novemba, 2025

Hafla ya uapisho wa Waziri Mkuu Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itafanyika Ikulu Chamwino, mkoani Dodoma, saa 04:00 asubuhi.

Sharifa B. Nyanga
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu


Soma pia Dkt. Mwigulu Nchemba apendekezwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

1763033740241.png
 
Anastahili Jembe la UDSM waziri mkuu wa kwanza Msomi
 
Back
Top Bottom