Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
Amani iwe nawe Mama yangu.
Heri ya sikukuu ya Eid! Na Polee na uchovu wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadan.
Kama nilivyotoa commitment ya kukuunga mkono Mara tu ulipochukua kiti cha kuongoza nchi yetu, leo napenda kuleta mada nyingine ya ushauri kwako ili tuutumie katika kuijenga na kuipeleka mbele kimaendeleo Tanzania yetu.
Hivi Karibuni, Botswana na Zambia wamezindua daraja la kuunganisha nchi zao linalojulikana kama Daraja la Kazungula. Daraja hili lililojengwa katika Mto Zambezi Lina njia za Magari kwa ajiri ya Magari na Pia wameweka sehemu ya kupitisha reli kwenye njia hii.
kukamilika kwa Daraja hili inaelezwa kuwa ni fursa adhimu ya kiuchumi kwa nchi zenye Bandari kuu za bahari hasa South Africa, Namibia na Tanzania kwa sababu daraja hili litazifanya hizi nchi kufanya biashara kwa kiwango kikubwa sana na kwa urahisi sana.
Tukiacha Namibia na South Africa , kwa Tanzania , nimeona kukamilika kwa daraja hili ni fursa kubwa sana ya kukua kiuchumi kwa Taifa letu endapo tu tutatumia hii kama fursa na kujitengeneza ki strategically hasa ukizingatia tukijipanga vizuri, mizigo yote ya Botswana na Zambia kutoka Middle East na Mashariki ya Mbali hasa Ulaya Mashariki na Asia( China na Japan) inaweza kuwa inapitishiwa Bandari zetu( Dar es Salaam na Bagamoyo Kama itajengwa) na kupelekwa kwao.
Hivyo kutokana na hii fursa, naomba serikali yako ianze kujipanga kufanya yafuatayo either yenyewe kama yenyewe au kwa kushirikiana na sekta binafsi.
1. Kujenga Bandari kubwa Kavu katika Mkoa wa Mbeya au Songwe, itakayokuwa inapokea mizigo yote Kwa ajiri ya nchi za DRC, Zambia, Zimbabwe na Botswana. Bandari hii itapokea mizigo hiyo kwa njia zote( Barabara na Reli kutoka Dar es Salaaam na Bagamoyo hapo badae
2. Kujenga upya miondombinu ya Mikoa ya Songwe na Mbeya. Naomba kwenye kufanikisha hili Mama yetu, angalia hata Kwa kufanya kupitia PPP( Kushirikiana na sekta binafsi) miundombinu ya kuingia Mbeya na Songwe hasa barabara ifumuliwe na kujengwa upya kwa viwango vya kisasa. Miji hii ina barabara nyembamba sana. Kuanzia Makambako hadi Mbeya na Songwe. Naomba mipango na utekelezaji uanze kufumua na kuzijenga kisasa katika viwango vipya vya ubora barabara hizi. Kwenye upana kuanzia makambako hadi songwe( Tunduma) na kuweka barabara zenye njia 3-4 kila line kwenye miji ya Mbeya na Tunduma ili kurahisisha usafiri wa abiria na mizigo. Kumbuka Mama njia hii ndo imeshika uchumi wa usafirishaji kwa Tanzania.
3. Mpango wa kuibadilisha reli ya TAZARA kutoka ilivyo kuwa SGR inayotumia umeme. Naomba kwa mipango ya badae reli hii inayofika Hadi Zambia iangaliwe kubadilishwa iwe kwenye mfumo wa SGR. Iboreshwe na kujengwa upya kisasa kwa viwango vipya vya ubora (SGR)
Mwisho ingawa wazo hili linaweza kuonekana la kufikirika zaidi kuliko uhalisia naomba Serikali yako ianze kufanya mipango ya kujenga daraja linalokatisha Ziwa Tanganyika na kuingia Congo Moja kwa Moja. Ninajua Kuna changamoto kubwa sana hasa kwenye kina cha lile ziwa Ila kwa kiwango cha teknolojia kilivyofika duniani Nina uhakika wapo watu wanaoweza kufanikisha hili. Ikiwa tutajenga kwa upande wa Rukwa sawa na ikiwa tutajenga kwa upande wa Kigoma sawa Ila naomba iyo mipango ianze sasa. Hata usipokuja kujenga wewe kama Rais wa Awamu ya Sita ila siku moja Rais mwingine atajenga tu. Kikubwa naomba uanzishe hiyo mipango kwa hata kufanyika feasibility studies na kuangalia ni watu gani wataweza kufanya hivyo huko mbeleni. Nasema hivi Kwa sababu, kama Tanzania, tukiweza kupata direct access ya kuingia Congo kibiashara itakuwa na faida kubwa sana kiuchumi kwa Taifa letu kuliko kutegemea kuingia kule kupitia nchi zingine jirani.
Naomba kuwasilisha.