Rais Samia, kuna Fursa nyingine huko 'Kazungula Bridge'


Hii ni biashara. Kama biashara itaonekana inawalipa wanaokuja Dar, kwanini isiwezekane? Sasa hivi Durban ndio reliable port. Ni mbali kweli kweli. Beira ugaidi na mapigano ya ndani yanaifanya isiwe rafiki sana
 
Humu JF ndio home of all ngazi za maamuzi..hata usiogope wapo wengi tu nanasoma na kuchukua taarifa..hata kwenye uzi wa kula kimasihala wapo.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ni biashara. Kama biashara itaonekana inawalipa wanaokuja Dar, kwanini isiwezekane? Sasa hivi Durban ndio reliable port. Ni mbali kweli kweli. Beira ugaidi na mapigano ya ndani yanaifanya isiwe rafiki sana
Unaemuelewesha sidhani kama anajua lolote juu ya biashara hasa baina ya mataifa
 
Hapo mwishoni nakubaliana na wewe kuhusu Bandari ya Dar es Salaam kutomudu changamoto tulizo nazo kwa sasa!

Msisitizo uwekwe Bandari ya Bagamoyo ili tuweze ku dominate biashara katika ukanda wetu huu na investiment kubwa ifanywe zaidi kwenye kujenga Bandari kubwa za kisasa mikoa ya mipakani na kuboresha miundombinu hasa ya reli na barabara kuelekea nchi jirani
 
Asante Ndugu
 
Nimekusoma mkuu, nikakumbuka ahadi ya kukutana nawe tena.

Hongera kwa maono yanayoelezwa na mstari huo hapo juu!
Hahahaaaa pa1 mkuu #Kalamu1


I'm here to stay .
 
Huu ni utajiri uliopo wazi kwa nchi yetu, lakini hatuuchangamkii ipasavyo sijui kwa nini!
 
Mambo mazuri na ya kimkakati kwa ajili ya maendeleo ya nchi yanapangwa na kuchagizwa na sheria zilizo bora kabisa. Mambo yote haya yanapangwa na viongozi wa kisiasa kwa kufuata ushauri wa wataalam.

Badly enough; kule Bungeni viongozi wapo bize kuwarushia Mbowe na CDM vijembe na kusahau kilichowapeleka Bungeni.
Unakaa unajiuliza kwanini Mizigo mingi inapitia Zambia kuingia Congo? kwamba miaka yote serikali inashindwa kujenga Bandari na kuweka Meli kubwa hapo ziwa Tanganyika?
Miaka mingi barabara ya TABORA-SIKONGE-MPANDA imekua tabu kwelikweli.
Barabara ya TABORA-KALIUA-NJIAPANDA YA UVINZA-MPANDA nako tabu tupu.

Alafu wengine wakaenda mbali zaidi wanajenga daraja la Salander kweli? wakajenga uwanja wa ndege pale Chato kweli?
Wakajenga Lami kutoka Namanyerere adi kibaoni kwao Pinda kweli? na umuhimu wa kuunganisha Katavi..Tabora na Congo inazidi umuhimu wa Salander na Chato Airpot.

Majuzi nilikua pale boarder Kasumulu Kyela na Malawi; sasa unajiuliza boarder inajengwa alafu barabara imebaki nyembamba kama mkia wa kiboko.
Viongozi wetu jirekebisheni muangalie kinachoweza kuungamisha fursa kwa wananchi wetu.
Chato ata mabasi ya abiria yenyewe hawapati wasafiri itakua ndege?
 
Good analysis

Umeeleza vyema Sana na nafurahi kuona ukiwa na mawazo chanya kwa mustakabali wa Taifa letu .

Nimefurahi kuona ulichokuwa unakipinga kule ndicho ulichokiungamkono huku ,kule niliamua kusitisha mjadala Baada ya kubaini kuwa wewe ni mkongwe mwenzangu humu ,much kudos jombaa.

Wewe jamaa uko na akili sana basi tu vile unaamuaga [emoji3][emoji3][emoji3]
 
Unaonekana hukuelewa chochote nilichokuwa napinga kule.
Lakini najua kwa nini ulizima ubongo wako ili usinielewe, kwa sababu mada ile uliyoianzisha ilikuwa inaeleza kila kitu juu ya ulikonadisha akili yako.
 
Unaonekana hukuelewa chochote nilichokuwa napinga kule.
Lakini najua kwa nini ulizima ubongo wako ili usinielewe, kwa sababu mada ile uliyoianzisha ilikuwa inaeleza kila kitu juu ya ulikonadisha akili yako.
[emoji1787]
 
Mkoa wa Mbeya umelaza sana damu kwani hawajaweza kucapitalize economic potential ya kufanya biashara na Malawi!!
Uchumi wa Tanzania unashikwa na biashara na nchi za Zambia, Malawi, Congo na Zimbabwe. Huku ndo mizigo Mingi inaenda alafu ukiangalia kwa kina hii ndo mikoa iliyosahaulika zaidi kimiundombinu pamoja na Tabora na Kigoma.

Kusema kweli ukifikiria kwa kina Reli ya TAZARA ndo ilitakiwa kuboreshwa zaidi na kufanywa kuwa SGR huku ikiwekewa umeme kutokana na hii reli ndo inayoenda kwenye njia yenye uchumi wa Tanzania.

Napendekeza Mama Samia aiangalia sana hasa kwenye kuiboresha kimiundombinu mikoa ya Mbeya na Songwe kuanzia kwenye barabara hadi kwenye reli.

Hii ni mikoa ambayo hata serikali ikiamua kufanya ujenzi wa miundombinu kwa mfumo wa PPP kuna uhakika wa faida kurudi mapema na kwa wakati kwa sababu huku uchumi ni usafirishaji na biashara.
 
Umeongea maneno mazito sana ndugu yangu. Malawi kwa walipo kijiografia kila kitu wanatakiwa kutegemea kutoka Tanzania. Kwa sababu hiyo sisi ndo tunatakiwa kulionesha Hilo na kulisimamia kwa kuhakikisha Kuna miundombinu Bora na ya kisasa zaidi kuingia Malawi. Barabara kuwa na viwango vya ubora, upana mzuri na wa uhakika bila kusahau miundombinu mingine.

Kwa mpaka wa Tunduma hali inatakiwa kuwa ivyo ivyo. Barabara zoote za kuingia Mbeya hadi Songwe zinatakiwa ziwe na Upana unaotakiwa na ubora unaotakiwa, reli ya TAZARA inatakiwa kuwa kiwango cha SGR na iwekewe kabisa umeme. Tukifanya hivi ndo Kweli tutakuwa serious kwa maendeleo ya kweli ya Tanzania.
 

Sahihisho dogo: kigezo rasmi cha SGR (Standard Gauge Railway) ni urefu kati ya reli ya kushoto na kulia (gauge) ambayo ni sentimita 1,435. Unaweza kufananisha na urefu wa axle ya magurudumu ya treni. Njia inaweza kuwa au isiwe ya umeme.

TAZARA imejengwa kwa kigezo cha Cape Gauge (sentimeta 1,067). Hii ndiyo gauge ya mtandao wote wa reli kusini mwa Afrika kuanzia Zambia hadi Cape Town. TAZARA iliunganishwa na mtandao huu kwa kusudi maalum. Ni kampuni binafsi ya GAUTRAIN ya Afrika ya Kusini pekee ndio yenye mtandao wake wa SGR ndani ya nchi hiyo kwa huduma ya abiria.

Bila shaka naamini ulitaka kusema miundombinu ya TAZARA iimarishwe na njia kuwekewa umeme lakini si kuibadilisha kuwa SGR. Lengo la uzi lingepotea.
 
πŸ‘πŸ‘πŸ‘ Ulivyoanza kulizungumzia hili kwa kulinganisha ndio umenifumbua macho, mitazamo yenye fikra pana namna hii ndio inayobadilisha mambo makubwa kuwa mazuri na kwa muda mfupi, inshallah natamani uzi huu uonwe na wenye vyeo vyao.
 
πŸ‘πŸ‘πŸ‘ Ulivyoanza kulizungumzia hili kwa kulinganisha ndio umenifumbua macho, mitazamo yenye fikra pana namna hii ndio inayobadilisha mambo makubwa kuwa mazuri na kwa muda mfupi, inshallah natamani uzi huu uonwe na wenye vyeo vyao.
Ebu fikiria Lami inayoishia Kibaoni kwao Pinda unaweza kukaa bale barabarani masaa zaidi ya matatu bila kuona gari wala pikipiki ikipita kwenye hiyo barabara...unajiukiza ilijengwa kwasababu Pinda ni Waziri mkuu?

Je barabara na daraja lililokua linaunganisha Tabora na Katavi imelaza watu njiani miaka mingi sana. Sehemu ya masaa matano watu wanakaa siku mbili barabarani na ni njia ya kufungua uchumi wa nchi na nchi achilia mbali mkoa kwa mkoa.
Ukibahatika kutembea ndani ya nchi hii unaweza kushangaa mengi sana.

Chukulia ile boarder ya kuunganisha Kenya na Tanzania upande wa Rorya - Shirati. Upande wa Kenya wamejenga majengo yao vizuri na wanakusanya mapato ila upande wa Tanzania shida kwelikweli. Licha ya ushauri uliokwisha tolea na ofisi ya CAG kuhusu ujenzi wa hizi boarder.
 
Sometimes nafikiria soln ni radical amendment kwenye utawala mzima, yaan nchi izaliwe upyaaaa!
Maana madudu yapo mengi mnoo na kwa viongozi dawa yao ndio hiyo fyeka fyeka kila kitu ila kwa wananchi sio sana coz baadh hawana elimu ambapo wakielimishwa mambo yanakuwa sawa ila kwa wasomi-viongozi ambao ni stiff-necked na waroho soln ni radical eradication shenz, mi nachukiaga kabisa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…